Kibondo
Shule ya msingi Kasebuzi wilayani Kibondo mkoani Kigoma inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa maji kwa ajili ya matumizi ya kuwapikia wanafunzi na huduma nyiongine za kiafya.
Hayo yamebainishwa wiki hii na wanafunzi waliohitimu elimu ya msingi shuleni hapo katika risala iliyosomwa nao wakati wa sherehe ya mahafali ya darasa la saba shuleni hapo.
Wanafaunzi hao wamebainisha kuwa shule inahitaji teknolojia ya uvunaji wa maji ya mvua katika majengo ya shule ili kupunguza tatizo hilo.
Wakisoma risala hiyo kwa niaba ya wenzao, Sikudhani Kazoya na Zubeda Issa wamebainisha kuwa kwa sasa shule inategemea kisima kimopja kilichopo kijijini humo ambacho hutumiwa pia na wanakijiji.
Aidha wanafunzi hao waliohitimu darasa la saba shuleni hapo wamechangia kiashi cha shilingi elfu kumi kwa ajili ununuzi wa vyombo vya kuchotea maji ili wanafunzi waliowaacha wasikose huduma ya chakula kwa kukosa maji.
Kwa upande wake mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kasebuzi Bi. Ester Nchukiranye amesema kwa kushirikiana na wananchi shule inaendesha zoezi la ufyatuaji wa matofali ili kuongeza nguvu mikakati ya shule ya kujenga madarasa na nyumba za walimu.
Naye mratibu miradi wa shirika la elimu la SAEU (Southern Africa Exitension Unit) Bw. Christopher Nkwezi ambaye alikuwa mgeni rasimi katika mahafali hayo amewataka walimu kuona fahali watoto wanapofanya vizuri katika mitihani yao.
Amehimiza pia suala la ubunifu kwa walimu na kuwapatia changamoto ya kuandaa mashindano katika mitihani ya kila mwezi ili kuwapima uwezo wanafunzi katika madarasa yao.
Aidha Bw. Nkwezi amewahimiza wazazi kuhakikisha hawakati tamaa ya kuwasomosha watoto wao na ameto wito kuwa wanafunzi wote waliohitimu darasa la saba wapelekwe katika shule za sekondari hata kama wizara haitawachagua wote.
Amewataka wanafunzi waliohitimu kutoona kuwa elimu ya msingi ndio mwisho wa kupata elimu badala yake watamani sana kuendelea hadi elimu ya juu ili wawe msaada mzuri kwa jamii na mfano wa kuigwa na wadogo zao.
Shirika la SAEU Kibondo linajenga shule ya sekondari ya kutwa kama sehemu ya kuisaidia wilaya hiyo kupunguza idadi kubwa ya watoto wanaokosa nafasi ya kujiunga na elimu ya sekondari kila mwaka