Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbunge, mkewe wazusha mambo Z’bar
Mbunge, mkewe wazusha mambo Z’bar
By Habari Tanzania | Published  10/25/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

MZOZO kuhusu gari la ubunge, umesababisha kuvunjika kwa ndoa ya Mbunge wa Kwamtipura, Zubeir Ali Maulid (CCM), na mkewe, Fatma Ali Ame.

Hayo yalitokea wakati mbunge huyo akiwa Tanzania Bara kwenye shughuli za kamati ya Bunge, na kuagiza gari hilo na jingine yapelekwe matengenezo, huku mkewe akitaka aendelee kulitumia kwani alishatia mafuta.

Gari lenyewe ni aina ya ‘Rav 4’, lenye thamani ya zaidi ya sh milioni 15, ambalo limeishia kuvunjwa kioo cha mbele, baada ya kuzuka mzozo, wakati dereva wa mbunge huyo alipokwenda kulichukua nyumbani kwa mkewe mbunge.

Hayo yalitokea Oktoba 17, nyumbani kwa Maulid, Mwanakwerekwe, Mkoa wa Mjini Magharibi, Unguja. Tayari tukio hilo limeripotiwa katika Kituo cha Polisi Mwanakwerekwe.

Akizungumza jana, mke wa mbunge huyo alisema kwamba siku ya tukio, alichukua gari hilo na kulitumia kwa shughuli zake za kikazi, lakini baada ya kurejea nyumbani, dereva wa mumewe alitaka kuchukua gari hilo ili alipeleke matengenezo.

“Kwa kuwa tayari nilishaweka mafuta ya zaidi ya sh 16,000, nilihoji nitafanyaje kazi, na kuamua kumpigia simu Mheshimiwa na kumtaka anipatie talaka yangu, kwa vile kitendo hicho kilikuwa ni kuendeleza manyanyaso dhidi yangu,” alisema Fatma.

Aliongeza kuwa, wakati akitafakari kitendo cha kunyang’anywa gari hilo kabla ya kumaliza shughuli zake, alifika mdogo wa mbunge huyo, na kuanza kufunga lango kuu la nyumba kwa kufuli, ndipo Fatma alitaka kujua sababu ya kuchukuliwa hatua hiyo.

Alisema mbali na tukio hilo, kijana huyo alianza kufungua matairi ya gari jingine lililokuwapo katika nyumba hiyo na ndipo ugomvi ulipoanza kati yake na shemeji yake.

Fatma alieleza kujeruhiwa sehemu za tumbo na mikononi na baadaye kupatiwa fomu ya matibabu kutoka Kituo cha Polisi cha Mwanakwerekwe na kutibiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja mjini Zanzibar.

“Nilipompigia simu kumwambia aliyemtuma achukue gari aje pia na talaka yangu, ndipo muda mfupi alipokuja shemeji huyo na kunishambulia vibaya sana kwa kunipiga,” alisema Fatma ambaye ni mfanyakazi wa Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB).

Alisema kwamba wamekuwa na matatizo ya kifamilia na mumewe kwa muda mrefu na tayari alishafungua malalamiko Wizara ya Wanawake na Watoto Zanzibar, lakini hadi sasa hakuna hatua zilizochukuliwa kutokana na matatizo yao.

Akizungumzia tukio hilo, Mbunge huyo wa Kwamtipura alisema ni kweli wana matatizo ya kifamilia na mkewe huyo na tayari ameshamuacha.

Alisema akiwa safarini Tanzania Bara kwa shughuli za kamati za Bunge, aliamua kutuma fedha kupitia katika akaunti ya mkewe mdogo ili magari yote yafanyiwe matengenezo.

Hata hivyo, alisema baada ya fedha hizo kumfikia dereva wake, alifanya juhudi ya kumtafuta mkewe kwa njia ya simu ili aruhusu magari hayo yakatengenezwe, lakini hakuweza kupatikana licha ya kumtuma dereva kazini kwake.

Alieleza kwamba baada ya dereva huyo kwenda kuchukua gari ili alipeleke matengenezo, ndipo ugomvi mkubwa ukatokea, kisha akamtuma mdogo wake kuweka mambo sawa.

“Ni kweli mwenzangu, baadaye niliona akinitumia ujumbe wa simu akiomba talaka, lakini kwanza nilichukua tahadhari ya kuondoa vitu vya thamani, kwa vile namfahamu anapokasirika huvunja vunja vitu,” alisema mbunge huyo.

Alisema hadi sasa mdogo wake amefunguliwa kesi polisi kwa madai ya kumpiga mtalaka wake huyo.

Waziri wa Kazi, Ajira, Maendeleo ya Wanawake na Watoto, Asha Abdallah Juma, alithibitisha kupokea kesi iliyowasilishwa na mke wa mbunge huyo, hata hivyo hakuwa tayari kuielezea zaidi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Mgharibi, Bakar Khatib Shaaban alithibitisha kuwapo tukio hilo na kwamba polisi wanaendela na uchunguzi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.