Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Trafiki kupunguza msongamano
Trafiki kupunguza msongamano
By Habari Tanzania | Published  10/24/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mohamed Mhina, wa Jeshi la Polisi

WIZARA ya Usalama wa Raia imesema kuwa, itaongeza idadi ya askari wa usalama barabarani jijini Dar es Salaam na miji mingine mikubwa yenye msongamano wa magari, ili kusaidia kazi ya kuyaongoza magari hayo kwa kubadilishana, kwa lengo la kupunguza msongamano.

Waziri wa wizara hiyo, Bakari Mwapachu alisema hayo jana baada ya kumaliza ziara ya ghafla ya kuzungukia maeneo yote yenye msongamano mkubwa wa magari barabarani aliyoifanya kwa helikopta.

Katika ziara hiyo iliyoanza saa 1:00 alfajiri hadi saa 3:00 asubuhi jana, Waziri Mwapachu alifuatana na Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) Saidi Mwema, Kamishna wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Alfred Tibaigana na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Polisi cha Dar es Salaam, Elice Mapunda.

Alisema kuwa doria hiyo ya helikopta itawezesha kuishauri serikali juu ya kupunguza tatizo la msongamamo na hata kutunga sheria na kuzifanyia marekebisho sheria zilizopo zihusuzo usalama barabarani.

Alisema kuwa, ujumbe wake umebaini kuwa tatizo kubwa la msongamano wa magari jijini Dar es Salaam, unasababishwa na matumizi mabaya ya barabara unaofanywa na madereva, wakiwamo wa mabasi ya daladala kupenyeza pembeni na mengine kusimama ovyo kwa kupakia ama kuteremsha abiria na miundombinu duni.

Ziara hiyo pia imebaini kuwa, barabara nyingi zimejengwa bila ya kuwekwa vituo vya kupakia na kuteremsha abiria, jambo ambalo linawalazimu madereva kukiuka sheria kwa kusimama ovyo katika maeneo yenye abiria kwa kupakia na kuteremsha.

Mwapachu pia alitumia fursa hiyo kuwaomba wadau na wananchi mbalimbali kuendelea kulisaidia Jeshi la Polisi kwa kuwapatia askari vyombo vya mawasiliano yakiwamo magari, pikipiki na redio call kwa lengo la kusaidia katika mapambano dhidi ya uhalifu.

Alisema kuwa baada ya kazi kubwa ya kupambana na majambazi na hali kuonyesha kufanikiwa, jeshi hilo sasa limeingia katika hatua nyingine ya kupambana na msongamano wa magari na ajali za barabarani.

IGP Mwema, akizungumza kwenye mkutano huo uliofanyika ofisini kwa Waziri Mwapachu, aliwaomba wananchi kuendelea kutoa taarifa mbalimbali zitakazoliwesha jeshi hilo kuendelea na mapambano dhidi ya wahalifu, wakiwamo wale wanaovunja kanuni na sheria za usalama barabarani


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by McFallan)
    Rating
    Ni vizuri kuelekeza nguvu za ziada katika kupunguza msongamano wa magari ndani ya majiji yetu. Hatua hii inastahili kupongezwa.
    Ila kwa upande wangu nafikiri pia kwamba ni vema serikali ikaangalia namna ya kuwa na barabara zinazoeleweka. Hili likienda sambamba na urekebishwaji wa sheria za barabarani itawezekana.
    Barabara nyingi za majiji yetu hususani Dar es salaam ni nyembamba, zenye mashimo, na zisizotengenezwa mara kwa mara. Pia barabara hizi hazina sehemu ya waenda kwa miguu, hazina sehemu ya waendesha baiskeli; mikokoteni, wanyama, binadamu, na magari wote/vyote kwa pamoja vinashiriki utumiaji wa barabara kwa pamoja. Hii haisababishi msongamano tu, bali inahatarisha usalama wa watumiaji wa barabara. Kuna nyakati pia viongozi wetu wanaibuka na mikakati ya kuzuia magari ya zaidi ya tani 3 kuingia mijini. Na fikiri hii sio suluhisho.
    Katika kutembelea nchi za wenzetu, naamini viongozi wetu wakuu wamekuwa wakiona uzuri na mpangilio wa barabara za huko. Je, kwa nini sio Tanzania? Mh. Waziri mkuu kwa mfano anaweza kutuambia nini kuhusu mipangilio ya barabara Johannesburg anakohudhuria vikao kwa sasa. Na viongozi wengine je?
    Suala ni maamuzi. Ni vema ukafika wakati baadhi ya nyumba ndani ya majiji zikabomolewa na kujengwa barabara. Tungekuwa na barabara, na kila nyumba ikawa na "access" na barabara, msongamano ungepungua tu. Maana badala ya kupitia barabara hii, utapitia nyingine.
    Mkakati mwingine, serikali inaweza kupanua jiji kwa kupeleka huduma muhimu nje ya Dar es salaam ya sasa. Mfano, huduma kama maofisi ya serikali yanaweza kuhamishiwa Kimanzichana. Kukapimwa vizuri, barabara zikajengwa tena pana na zenye lami. Hii itafanya badala ya watu kwenda city centre ya sasa wakaenda city centre ya baadae na hivyo, kupuguza msongamano.
    Barabara nyinginezo zilizo nyembamba sana kama za Tabata, ukosefu wa taa za barabarani, uendeshwaji wa Daladala unaofanywa na "dai waka" ni sehemu ya tatizo pia.
    Kuhusu mambo mengineyo yanayoweza kushughulikiwa inaweza kuwa ni pamoja na madereva kuelimishwa zaidi juu ya nani apite kwanza. Mfano, nchi kama New Zealand; mara nyingi sana unless kama kuna alama inayokuambia kufanya vinginevyo, "unapisha gari inayotoka kulia kwako" ipite kwanza. Pia huko NZ sheria ya barabarani ni msumeno kwa maana kwamba, hata mwenda kwa miguu akikosea na ukamgonga, anawajibika. Tanzania wewe mwenye gari ndo utaipata labda uzime kesi kwa kuhonga matrafiki.
    Isitoshe, barabara zetu hazina alama za barabarani, hakuna hata misitari iliyochorwa barabarani kuwasaidia watumiaji wa barabara.
    Kusema kweli, ipo kazi. Mpaka nguvu za pamoja zitumike kuikwamua nchi.
    Kwa wale waliokwisha safiri safiri nje ya nchi, watakubaliana nami kwamba barabara zetu za Tanzania; katika majiji yetu; zinazidiwa na barabara za uchochoroni za nchi za wenzetu. Pengine tutasema sisi ni maskini. Maana hili ndo limekuwa kama kisingizio. Je, umaskini hata katika "planning" je, umaskini huu ni wa aina gani? Mbona Tanzania inawasomi wa kutosha? Mbona mambo mengine ni madogo kiasi kwamba hatuhitaji kusaidiwa na weupe au mashirika ya misaada? "Issue"hapa ni kuamua kuwa wawajibikaji.
    Kuna nyakati hufikiri kwamba, labda, udikteta wa aina fulani unafaa ili watanzania tuamke.
    Mara nyingi watu waliokabidhiwa dhamana wanatanguliza matumbo yao na sio maslahi ya nchi. Wanajenga barabara chini ya kiwango, mfano Morogoro, kisha wanaachwa waendelee kupeta. Tungefikia kiwango cha sheria kuwa sheria, kuwafunga hata wamiliki wa "Enrons" za Tanzania.
    Inatia uchungu sana
     
Submit Comment


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.