Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mwanafunzi kidato cha kwanza atengeneza ndege na kuirusha angani!
Mwanafunzi kidato cha kwanza atengeneza ndege na kuirusha angani!
By Prosper Kwigize | Published  10/24/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Kibondo
 
Mwanafunzi mwingine wilayani Kibondo amefanikiwa kukiweka hadharani kipaji chake cha ajabu baada ya kutengeneza ndege na kuirusha angani kwa mara ya kwanza na kuiacha jamii midomo wazi.
 
Kijana huyo mwenye umri wa miaka 17 Omary Birapfumba, anayesoma kidato cha kwanza katika shule ya sekondari ya Moyowosi wilayani hapa ameibuliwa na mwandishi wa habri hiii alipotembelea katika shule hiyo wiki hii.
 
Ndege hiyo yenye ulefu wa takribani futi tatu na upana futi moja na kimo sentimeta arobaini iliyoundwa kwa kutumia boksi na plastiki na kuwekewa vifaa kadhaa ndani pamoja na injini iliruka kimo cha karibu mita 50 juu kisha kuondoka moja kwa moja angani.
 
Wanafunzi na wafanyakazi kwa ushirikiano na walimu wa shule hiyo waliokuwepo wakati wa jaribio la kijana huyo walijaribu kwa kuirushia ndege hiyo mawe kwa nia ya kuishusha chini lakini jitihada zao ziligonga mwamba huku wakikimbia nayo mstuni.
 
Kijana Birapfumba akitumia ujuzi wa kisayansi zaidi kuliko nguvu aliwatia moyo walimu na wanafunzi wake kuwa ndege hiyo isingefika mbali kutokana na kwamba injini yake inatumia betri ndogo aina ya National Panasonic na kwamba ingeanguka chini kwa kukosa nguvu.
 
Akielezea sababu za ndege yake kuruka moja kwa moja kijana Omary Birapfumba alisema, ilitokana na hitirafu katika chombo cha kuiongozea maarufu kama rimote ambayo anaitumia katika kuongoza injini ya ndege hiyo.
 
Hata hivyo mwanafunzi huyo ambaye anadaiwa kukaa tumboni mwa mama yake kwa kipindi cha miaka miwili kabla ya kuzaliwa badala ya miezi tisa, amefanikiwa pia kuonesha mashine ya kufua umeme maarufu kama genereta ambayo nayo iliweza kufanya kazi.
 
Akielezea namna alivyofanikiwa kuunda chombo hicho cha usafiri ambacho ni adimu kwa watanzania kukiunda,  kijana Birapfumba alisema yeye tangu akiwa mdogo amekuwa akijishughulisha na masuala ya ubunifu.
Alifafanua kuwa licha ya kubuni na kuunga zana hizo za usafiri na uzalishaji wa umeme, tayari amefanikiwa pia kuunda mtambo wa kuvuta mawimbi ya sauti na picha za video ambapo wakazi wa kijiji cha Kifura anakoishi ambao wanamiliki runinga wameweza kupata matangazo ya ITV, Star TV, TVT na Chanel Ten.
 
Mwandishi wa habari hii anaendelea na uchunguzi zaidi ili kujua kwa undani jinsi kijana huyo alivyo fanikiwa kuunda zana hizo ikiwa ni pamoja na kuwaibua vijana wengine zaidi ambao wanavipaji ambao hawajatangazwa.
 
Hii ni mara ya pili kwa vijana wanaosoma shule za sekondari wilayani Kibondo kuunda mitambo kama hiyo baada ya kijana Eliud Kajuni aliyemaliza kidato cha nne mwaka huu katika shule ya sekondari Maragalasi wilayani Kibondo kuunda mitambo ya Radio na kufanikiwa kurusha matangazo kwa umbali wa kilomita tatu

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by JOHN)
    Rating
    Hakika hii sasa ni changamoto kubwa kwa serikali, nadhani sasa Kigoma kuna vipaji vya ajabu na kuna haja ya mamlaka ya mawasiliano Tanzania kwenda kushirikiana na mwandishi huyu kuibua vipaji, haitakuwa vema kuona au kusikia eti serikali inawaijia juu vijana hawa wa Kibondo bali inapaswa kutoa ushirikiano kwao na ikiwezekana muwasaidie vijana hao. Kazi njema Prosper Kwigize keep it up

     
  • Comment #2 (Posted by matata Mudeshi)
    Rating
    sasa naona kuna haja ya vija hawa wenye vipaji kusaidiwa, maana nchi yetu inahitaji sana wataalamu na wabunifu ambao watasaidia kukua kwa teknolojia na kupunguza tatizo la tanzania kuendelea kutegemea wataalamu na wavumbuzi kutoka nje ya nchi, matatizo ya ajila kwa vijana yatapatiwa ufumbuzi iwapo Tanzania itakubali kuwa sisi pia (watanzania) tunaweza kuliko kutegemea wazungu tu.

    Nampongeza sana kijana huyo wa Kibondo kwa ubunifu na majaribio yake.
     
  • Comment #3 (Posted by antony)
    Rating
    Mkoa wa Kigoma jivunieni kipaji cha ajabu walichonacho vijana wenu na anzisheni mkakati wa kuwaendeleza, kwa kuwakubali kwanza na kisha kushirikiana nao, Kwa pamoja tutaikomboa tanzania na utumwa wa teknolojia
     
  • Comment #4 (Posted by Msifuni Mmasa)
    Rating
    Please,let uplift the founder by giving himm full support on his initiatives
     
  • Comment #5 (Posted by pockey)
    Rating
    hii ni muhimu kuelimishana lazima serikali iunde mbuni bunifu ya kuwaendeleza vijana hawa
     
  • Comment #6 (Posted by joseph)
    Rating
    Hakika Tanzania ina kila sababu ya kuona fahali, vipaji vya hawa watoto wawili wa Kibondo ni lazima viangaliwe kwa mazo ya ziada si tu kuwasifu kwa maneno bali kwa vitendo, kuna haja ya watanzania wote wanaopata au kusoma habari hii wawaze mara mbili je hawa wangekuwa ni watoto wetu au wadogo zetu tungefanya nini, basi kwa kuwa labda watoto wetu hawana au hawajaonesha vipaji vyao basi tubuni chochote cha kuwasaidia au kuwainua ili wawasaidie watanzania na vijana wenzao, Mamlaka ya mawasiliano Tanzania hii ni changamoto kubwa kwenu si tu kuratibu masuala ya mawasiliano bali pia muwe na moyo wa uzalendo kwa vijana hawa, wasaidieni sana, nisingependa kusikia eti mnaona uchungu na kuwazuia kujaribu zana zao, badala yake ebu wapeni mbinu na msaada ya kiuchumi na kiteknolojia zaidi ili tuondokana na dhana ya kudhani kuwa WAZUNGU TU WANAWEZA.

    HABARITANZANIA.COM kwa fahari ya mtandao wenu kuwaibua vina ahawa waili yule wa radio na huyu wa ndege basi fungueni japo ukurasa wa FUNDRISING kwa ajili yao ili wenye moyo wawasaidie vijana hawa walau hata tu kuwasomesha shule za wenye vipaji maalumu, au kuwatembeza japo katika viwanda na IT place za ndani na nje kwa nia ya kupanua wigo wa mitazamo yao kisayansi, Lakini pia epu andikeni japo makala kwenda kwa UNESCO ili nao waweze kuwasaidia vijana hawa. asanteni sana.
     
  • Comment #7 (Posted by NJIWA)
    Rating
    WOW
     
  • Comment #8 (Posted by Mesiaki Ilmolelian)
    Rating
    Wavumbuzi wote huku ulaya na Marekani kama kina Albert Einstein, Bell wote ni kama wamezaliwa na vipaji. Hivyo Chuo Kikuu cha DSM n.k kwa kutumia taasisi zao za utafiti wawe karibu na watu hawa wenye kiu ya kuvumbua au hata kuboresha technolojia.
     
  • Comment #9 (Posted by Singo)
    Rating
    Vijana kama hao ni wa kusaidiwa sana na kutiwa moyo kuendeleza vipaji vyao. Tafadhali sana wasaidieni hao kupitia wizara ya Tech. na Elimu ya juu...Ni taifa la kesho hao jamani jamani...
     
  • Comment #10 (Posted by an unknown user)
    Rating
    Mplekeni Nyumbu JKT akasaidiane na engineers kuedeleza kile alichonacho
     
  • Comment #11 (Posted by Hadija)
    Rating
    serikali inatakiwa iwasaidie vijana hawa. watakuwa wanasayansi wa kesho. kulikoni kuleta ma tx kutoka nchi za nje....
     
  • Comment #12 (Posted by Hassan)
    Rating
    Kijana kafanya mambo si madogo serikari lazima imtupie macho ili kipaji chake kisipotee.

     
  • Comment #13 (Posted by Vitalis Temu)
    Rating
    It is not quite a new idear. All he did is to copy and enlarge what is there in toy planes.
    However, the student proved his strong IQ and him and several others need be promoted accademically.
     
  • Comment #14 (Posted by emeline mwasongwe)
    Rating
    is good
     
  • Comment #15 (Posted by John Paul)
    Rating
    Nimefurahi sana kuona kijana wa kiafrica anaweza kufanya mambo makubwa namna hii. Tumpe moyo na msaada wa aina zote. Huyu anatakiwa mfadhili asije akakwama popote. Lazima tuwe na system ya ku monitor asije kuwekewa kau zibe na mtu yoyote popote. Asante kijana keep it up!
     
  • Comment #16 (Posted by benedict)
    Rating
    The article is nice because it gives a challenge to ;
    1 .student who have talent should not hide ,let them be open to show the society.

    2 .journalist to explore the student who shows mirecle like that student from kibondo so that they keep up showing there
    art work .
     
  • Comment #17 (Posted by kassim kazi)
    Rating
    good job omar
     
  • Comment #18 (Posted by Frank Chacky)
    Rating
    should be encouraged by introducing him to the professionals.
     
  • Comment #19 (Posted by Eng.zuberi)
    Rating
    Tunahitaji udhibitisho!
     
Submit Comment


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.