Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  BET yafanya utafiti wa zao la pilipili Nzega
BET yafanya utafiti wa zao la pilipili Nzega
By Habari Tanzania | Published  05/29/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
HALMASHAURI ya Biashara ya Nje (BET) inafanya utafiti wa zao la pilipili aina ya Paprika katika kijiji cha Ngukumo, wilayani Nzega mkoani Tabora.
 
Kufuatia uamuzi huo, ujumbe wa Halmashauri hiyo jana ulifika kijijini hapo na kuzungumza na wananchi kuhusu azma yake hiyo na uwezekano wa kusaidia katika kuendeleza kilimo cha zao hilo.
 
Kiongozi wa ujumbe huo, Edwin Rutageruka katika mkutano wake na wanakijiji wa Ngukumo aliwaeleza kuwa utafiti huo ni muendelezo wa kazi iliyoanza kufanywa na taasisi ya Mandate Africa Foundation, miaka sita iliyopita.
 
"Eneo hili lina rasilimali nyingi, zikiwemo maji kutoka bwawa la Mihama pamoja na eneo kubwa la ardhi ambayo inapaswa kutumika kuwaendeleza kiuchumi badala ya kuendelea kubakia kuwa pori," alisema.
 
Endapo mradi huo utafanikiwa kuanzishwa, utaziwezesha jumla ya kaya 400 kujitegemea kiuchumi kutokana na ajira itakayotokana na kilimo hicho.
 
Zao hilo hulimwa kwa msimu kwa hivyo baada ya msimu kumalizika, mashamba yake yatatumika kwa ajili ya kuzalisha mazao mengine, mahindi kwa upande wa chakula na vitunguu, ambalo ni zao la biashara.
 
Alisema, sambamba na utafiti huo, pia BET kwa kushirikiana na Mandate Africa Foundation zitashirikiana katika kutafuta wawekezaji ambao wataendeleza kilimo hicho.
 
"Jukumu kubwa la wawekekzaji hao litakuwa ni kutafuta pembejeo na kununua vifaa vya umwagiliaji kutoka bwawa Mihama lililopo kijijini hapo, ambalo liko tayari kimatumizi kutokana na serikali kukamilisha mfumo wake wa usambazaji wa maji katika miaka ya 70.
 
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Mandate Africa Foundation, Bernadette Majebelle alisema utafiti wa awali kuhusu zao hilo umegundua kuwa mkoa wa Tabora una uwezo wa kuzalisha tani 2,000.
 
Alisema, licha ya kuweko kwa mahitaji makubwa ya Paprika, kiasi kinachozalishwa ni kidogo na kisichokidhi mahitaji katika soko la dunia.
 
Alitoa mfano ambapo alisema, mwaka 2003 kampuni ya Evesa ya Hispania ilitoa oda ya tani 10,000 lakini mahitaji hayo yalishindwa kutimizwa na badala yake ni tani 250 tu kutoka hapa nchini ndizo zilizoweza kufikishwa sokoni hapo.
 
Sambamba na Tanzania, nchi nyingine zinazozalisha Paprika ni Afrika Kusini, Zimbabwe na Zambia.
 
Kutoka gazeti la Uhuru
ISSN 0876-3896 NA.19321
Na Khamis Hamad, Tabora

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.