Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kaya 641 zapewa wiki kuondoka msituni
Kaya 641 zapewa wiki kuondoka msituni
By Habari Tanzania | Published  10/22/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Milka Ezekiel, Singida
UONGOZI wa Serikali Mkoani Singida umetoa siku saba kwa wananchi waliovamia msitu wa hifadhi wa Minyughe waondoke, vinginevyo wataondolewa kwa nguvu.

Kaimu Mkuu wa Mkoa, Florence Horombe alitoa agizo hilo mwishoni mwa wiki wakati akizungumzia amri iliyotolewa kwa wananchi hao tangu Aprili mwaka huu.

Alisema tangu Aprili mwaka huu, wananchi hao waliamriwa na Mkuu wa Mkoa, Vincent Parseko Kone kuondoka katika hifadhi hiyo, lakini wamekaidi.

Hadi sasa, kaya 641 zimehamia katika hifadhi hiyo ya Miyughe, jambo ambalo Horombe alisema ni kinyume cha sheria.

Horombe ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ta Singida, alisema kaya hizo zimepewa hadi Oktoba 27 kuwa zimeondoka katika hifadhi hiyo ambayo ni rasilmali kwa mkoa na taifa kwa jumla


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.