Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Magufuli na Ardhi
Magufuli na Ardhi
By Marshy Abdu | Published  10/21/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Magufuli na Ardhi

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, jana alimpa wakati mgumu Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Mulyambogo, na kumtaka awaeleze wananchi sababu zilizokwamisha ugawaji wa viwanja 3,000.

WAZIRI wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, John Magufuli, juzi  alimpa wakati mgumu Afisa Ardhi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo, Michael Mulyambogo, na kumtaka awaeleze wananchi sababu zilizokwamisha ugawaji wa viwanja 3,000.

Hatua hiyo pia ilimgusa Mkuu wa Idara ya Upimaji na Ramani wa Chuo Kikuu kishiriki cha Ardhi (Uclas), Martin Hagai, baada ya taasisi hiyo kutajwa na afisa ardhi huyo kuwa ndiyo ilipewa jukumu la kupima viwanja hivyo.

Katika kujitetea mbele ya mkutano wa hadhara uliofanyika juzi  kati ya Waziri Magufuli na wanakijiji wa Zinga, wilayani hapa, watendaji hao walijitia kitanzi kwa kumuahidi Magufuli kuwa baada ya wiki mbili, watakuwa wamekamilisha utaratibu, tayari kwa kuwakabidhi wahusika viwanja vyao.

Hali hiyo ilitokana na kero mbalimbali zilizowasilishwa katika mkutano huo baada ya wananchi kulalamika mbele ya waziri kuwa wamekuwa wakizungushwa na halmashauri hiyo kuwapatia viwanja ambavyo walivilipia tangu mwaka jana.

"Tulilipia viwanja kupitia Benki ya NMB tangu mwaka jana, lakini hadi sasa viwanja hivyo havijapatikana. Wakati ule tulipolipia, bei ya mfuko wa sementi ilikuwa Sh7,000 lakini sasa imefikia Sh10,000, sasa wanataka watukabidhi viwanja wakati bei imefikia Sh50,000," alisema Abadallah Majura, mmoja wa waathirika hao.

Kwa mujibu wa wananchi hao, bei ya viwanja vikubwa ilikuwa Sh300,000, vya kati Sh120,000 na vidogo Sh70,000. Akijibu hilo, Magufuli alisema, "Labda hili nimuulize afisa ardhi," na hapo hapo akamuita afisa huyo mbele ya umati wa watu waliohudhuria mkutano.

"Kwa nini watu wametoa fedha zao na mpaka sasa hawajakabidhiwa viwanja vyao?" aliuliza Magufuli na kushangiliwa na wananchi. Afisa huyo alisema kuwa kazi hiyo walipewa Uclas.

Afisa huyo wa Uclas pia aliitwa na kueleza kuwa mchakato wa kupima waliuanza Septemba mwaka jana. Aliyataja matatizo yaliyowakumba katika kupima maeneo hayo kuwa ni pamoja na mvua kubwa zilizonyesha, upinzani kutoka kwa wananchi ulioambatana na kuondolewa kwa vigingi.

Waziri huyo aliwasisitiza watendaji hao kutimiza ahadi yao ya kutoa viwanja ndani ya wiki mbili. "Kwa vile wameahidi mbele yenu, na Mungu anawasikia, viwanja 3,000 vitapatikana baada ya wiki mbili," alisema Magufuli na kuelekeza viongozi wa wilaya kufuatilia kwa karibu.

Tunakushukuru sana waziri Magufuli kwa kitendo chako hicho cha kutoa nafasi ya kuulizwa maswali na wananchi na wahusika kukubali makosa ila tunachokiomba utekelezaji huo uchukue nafasi yake zisiwe ni sound tu.

Ila tunaomba nchi hii na viwanja hivyo vinavyogaiwa na serikali viwepo katika mfumo mzuri wa miundo mbinu na kuwezesha nchi hiyo nayo kuwa na mitaa ambayo itasaidia kupunguza uhalifu na vilevile kufikiwa kiurahisi na wazima moto na polisi kwa hatari yoyote itakayojitokeza

Inasikitisha kuona waziri anakula kuku tu wizarani na huku raia tukilia njaa kutokana na uzembe wa watu fulani wanaojiona wao ni miungu watu katika serikali hiyo

Tunaendelea kumlalamikia waziri wa mambo ya ndani,na raisi wa nchi hiyo kwa ujumla kwa kukaa kimya huku Wamachinga ambao nao ni raia wa nchi wakifukuzwa kama mbwa na kuwakaribisha wageni ambao ni Wakenya na Wauganda katika shirikisho la umoja wa Afrika Mashariki,na kutaka kutuletea Wanyarwanda na Waburundi ambao wenyewe kwa wenyewe hawaelewani,

Waziri wa mambo ya ndani anaendelea kula kuku huku raia wa nchi ya China wakipiga raia na kufunga kituo cha polisi,wakuu wa wilaya wakichapa watu vibao vya kikelbu,polisi wakiendelea kunyanyasa raia

Tunakuomba muheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete wewe ndio mtu wa mwisho kuiteketeza ama kuinusuru nchi yetu hii tunakuomba hao mawaziri ambao unaona pia kazi hawaziwezi uwafukuze kama ulivyowafukuza hao waliopita

   AHSANTE.

 


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.