MFANYAKAZI wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Makao Makuu, Jason Katilihwa, amejeruhiwa vibaya na watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi, waliomvamia nyumbani kwake Mbagala -Charambe, Dar es Salaam.
Akizungumzia tukio hilo, mtoto wa mfanyakazi huyo aliyejitambulisha kwa jina la Jackline, alisema kuwa watu hao wapatao 30 walivamia nyumbani hapo na kumjeruhi.
Alisema watu hao kabla ya kuingia ndani walilipua kitu chenye mlio mkali na kusababisha nyumba kutikisika.
“Walianza kufyatua kitu chenye mlio mkali na kilisababisha nyumba ikatikisika ndipo walipoingia ndani na kumwamuru baba awape sh milioni 50 na ufunguo wa gari ili wasimuue, lakini aliwajibu kuwa hana, ndipo wakaanza kumshambulia kwa mapanga.
“Baada ya hapo wakaja chumbani kwetu na kutuamuru tuvue nguo ili watuingilie kimwili, lakini hawakufanikiwa kufanya hivyo, kwani tuliwashinda nguvu ndipo walipochukua panga na kumkata mdogo wangu mkono,” alisema Jackline.
Alisema baada ya tukio hilo, watu hao walitoa nje na na kuanza kupasua vioo vya gari.
Wakizungumza na Tanzania Daima, baadhi ya majirani walisema kuwa matukio kama hayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara, hivyo wameiomba serikali kuwapatia kituo cha polisi, kwani kilichopo sasa kipo mbali