Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mahita ashindwa kujitetea
Mahita ashindwa kujitetea
By Habari Tanzania | Published  10/21/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Happiness Katabazi

ALIYEKUWA Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Omari Mahita, ameshindwa kuwasilisha utetezi wake Mahakama Kuu katika kesi ya madai ya sh milioni 500 iliyofunguliwa na Chama cha Wananchi (CUF).

Wakili wa Mahita, Charles Simgalawa, aliiomba mahakama jana kuwa mteja wake ameshindwa kuwasilisha utetezi wake kwa muda unaotakiwa kwa kuwa alichelewa kupata nakala ya madai na kuongeza kuwa mteja wake hapatikani kwa urahisi, kwa kuwa ana makazi mengi ya kuishi.

Kutokana na hali hiyo, Jaji Laurean Kalegeya, anayesikiliza shauri hilo jana alishindwa kuendelea na kesi hiyo, hivyo kuahirisha hadi Novemba 11 na kumtaka Mahita kuwasilisha utetezi kabla ya tarehe hiyo.

Kwa mujibu wa hati ya madai, CUF inamshitaki Mahita kutokana na kukihusisha chama hicho na ujambazi, pia wanataka walipwe fedha hizo kwa kukituhumu chama hicho kuingiza nchini kontena la visu kwa ajili ya kuvuruga Uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge uliofanyika Desemba 14, mwaka jana .

Kesi hiyo ya madai namba 27/2006, imefunguliwa na bodi ya wadhamini wa chama hicho, na wanawakilishwa na Kampuni ya uwakili ya Taslima Law Chambers.

CUF wanataka walipwe fedha hizo kutokana na Mahita kuwakashifu kupitia vyombo vya habari, hali iliyowaondolea uaminifu wanachama wa chama hicho.

Inaeleza kuwa Desemba 13 mwaka jana, siku moja kabla ya kufanyika Uchaguzi Mkuu, Mahita alitoa taarifa za uongo kuwa wamekamata kontena la visu vilivyoletwa na chama hicho kwa ajili ya kuvuruga uchaguzi.

Hati hiyo inaeleza kuwa Februari 9 mwaka huu, akiwa katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay, jijini Dar es Salaam, alitamka kuwa chama hicho kinahusika katika wimbi la ujambazi.

“Kutokana na taarifa hizo, vyombo mbalimbali vya habari nchini viliandika taarifa hiyo.

“Siku iliyofuata gazeti la The Guardian ukurasa wa kwanza liliandika ‘CUF has hand in armed robberies’, Majira liliandika ‘CUF wanapanga ujambazi -Mahita’, Tanzania Daima liliandika ‘Mahita: CUF ni majambazi’ na Mwananchi liliandika ‘Mahita atoa mpya. Awahusisha CUF na wimbi la ujambazi’.

Wanaeleza kuwa habari zote hizo ni kashfa dhidi ya chama hicho.

Wanaeleza kuwa kashfa hizo hazina ukweli wowote na kwamba alikuwa na dhamira ya kukichafua chama hicho ili kionekane hakifai katika jamii, hivyo kinapaswa kuepukwa


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.