MKUU wa Mkoa (RC) wa Ruvuma, Monica Mbega, na wadaiwa wenzake wawili, kwa mara ya kwanza tangu wafunguliwe kesi ya madai ya kumtorosha mke wa mtu katika Mahakama Kuu ya Tanzania, jana walitinga mahakamani hapo.
Kesi hiyo ya madai ilifunguliwa na Hamis Mshindo dhidi ya Mbega, Edward Nziku na Maria Nziku. Kesi hiyo ilifunguliwa mahakamani hapo mwaka 2005 na kupewa namba 31/2005.
Kesi hiyo ipo mbele ya Jaji Juxton Mlay, imekwisha kutajwa mara tatu na wadaiwa walikuwa hawafiki mahakamani.
Jaji Mlay alimtaka mdaiwa wa pili ambaye ni baba wa mdaiwa wa tatu aieleze mahakama kwanini ameshindwa kuwasilisha utetezi wake na kushindwa kutoa taarifa za kutohudhuria mahakamani.
Mdaiwa huyo aliieleza mahakama kuwa yeye alikuwa Sumbawanga vijijini akitibiwa na huko alikokuwa akipata matibabu hakukuwa na vyombo vya mawasiliano, hali iliyosababisha kushindwa kupata taarifa kuhusu kesi inayomkabili.
Jaji Mlay, alimpa siku 21 kuanzia jana awe amewasilisha utetezi wake na kuahirisha kesi hadi Desemba 12.
Kwa mujibu wa hati ya madai, mlalamikaji anataka alipwe sh milioni 600 kwa ajili ya wadaiwa kumtorosha mkewe, ambaye ni mdaiwa wa tatu. Anadai kuwa mdaiwa wa kwanza alimtorosha mkewe, hali iliyosababisha kupoteza baadhi ya viungo wakati akimtafuta