Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Uingereza inawindwa zaidi na al-Qaeda
Uingereza inawindwa zaidi na al-Qaeda
By Habari Tanzania | Published  10/20/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

MAOFISA wa ulinzi wa Uingereza, wamesema nchi yao kwa sasa inawindwa zaidi na al- Qaeda, hasa baada ya shambulizi lililofanyika nchini humo, Julai 7, na kuua watu 52.

Maofisa hao wanasema hali imekuwa ya wasiwasi tangu kipindi hicho na kuwa ulinzi zaidi umewekwa kila mahali kuhakikisha kuwa mashambulizi zaidi hayatokei.

Wanaamini kuwa kwa sasa mtandao huo unaendeshwa kupitia vikundi vidogo vidogo vilivyoundwa ndani ya Uingereza, ambavyo vina silaha za maangamizi na kuwa mashambulizi ya Julai 7, yalikuwa ni mwanzo tu.

Vikundi hivyo kila kimoja kina kiongozi wake na vinashughulika na silaha za maangamizi, na vikundi hivyo vinafanya kazi katika maeneo tofauti na kuna kiongozi anayesimamia vikundi kadhaa kwa pamoja.

“Miaka mitano iliyopita ilikuwa ikifikiriwa kuwa al-Qaeda ni mtandao tu ambao haukuunganika, wenye lengo moja, lakini kwa sasa ni mtandao ambao umejipanga kwa namna ya ajabu,” anasema Crispin Black mchunguzi wa mambo ya usalama.

Wanausalama wana wasiwasi kuwa mtandao huo kwa sasa unajipanga kushambulia vyuo vikuu na taasisi nyingine za kijamii.

Hata hivyo, mchunguzi huyo amesema shambulizi lingine nchini humo kwa sasa sio rahisi kwa kuwa wanausalama wamejipanga vizuri.

Alisema wanausalama kwa sasa wanatambua ni nani wanayemtafuta na wamepewa mafunzo ya uhakika ya namna ya kupambana na wanamtandao hao.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.