Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Uchumi  »  TCCIA KIBONDO LAWAMANI
TCCIA KIBONDO LAWAMANI
By Prosper Kwigize | Published  10/19/2006 | Uchumi | Unrated
.Yadaiwa kudharau maagizo ya serikali
Chama cha wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda TCCIA wilayani Kibondo kimedaiwa kudharau maagizo ya serikali ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya chemba ya tarafa ya Mabamba.
 
Madai hayo yametolewa na mkuu wa wilaya ya Kibondo luteni kanali John Mzurikwao alipokuwa akijibu hoja ya kutotekelezwa kwa maagizo yake mengi juu ya maendeleo wilayani Kibondo.
 
Akiongea na Radio Kwizera juu ya TCCIA kutokamilisha ujenzi wa ofisi na ufunguzi wa matawi katika maeneo mengine, luteni kanali Mzurikwao amesema amesikitishwa sana na kitendo cha ukaidi wa wafanyabiashara hao.
Chemba ya wafanyabiashara, wenye viwanda na kilimo, mwezi wa tano mwaka huu walifungua tawi la umoja wao katika tarafa ya mabamba, katika hafla kubwa iliyohudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa, wilaya na mbunge wa jimbo la Muhambwe Felix Kijiko.
 
Katika hafla hiyo mkuu wa wilaya kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa Kigoma wa wakati huo Bibi. Halima Kasungu aliagiza ujenzi wa ofisi ya tawi aliloliwekea jiwe la msingi kukamilika katika kipindi cha mwezi mmoja, lakini hadi sasa hakuna kilichoongezeka katika jengo hilo.
 
Aidha sambamba na uzinduzi wa tawi hilo, TCCIA waliendesha harambee kubwa ya uchangiaji wa fedha kwa ajili ya ufunguzi wa matawi mengine katika mwambao wa mpaka wa Burundi na Tanzania, ambapo kiasi cha shilingi laki tatu zilichangwa na washiriki wa harambee hiyo.
 
Sambamba na hayo serikali iliwataka TCCIA wilaya, kuanza mara moja mikakati ya mawasiliano na wafanyabiashara kutoka nchi ya Burundi ili kuangalia uwezekano wa kubadilishana bidhaa.
 
Walitakiwa pia kuhamasisha wananchi kuchangia maendeleo ya chemba kwa kila kaya kujitolea kiasi cha shilingi mia moja ambazo zingesaidia ujenzi wa matawi na utoaji elimu kwa wafanyabiashara, wakulima na wenye viwanda.
 
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hii umebaini kuwa katika ahadi zilizotolewa na TCCIA pamoja na maagizo ya serikali hakuna kilichofanyika hadi sasa licha ya kujiingiza katika mpango wa mifuko ya akiba na mikopo SACCOS.
 
Licha ya kutafutwa, uongozi wa TCCIA hawakuweza kupatikana mara moja ili kujibu tuhuma hizo na juhudi za kuwatafuta zinaendelea ili kujua mwelekeo na sababu za kutotekeleza licha ya kupewa michango

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.