Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mshitakiwa afanya fujo mahakamani
Mshitakiwa afanya fujo mahakamani
By Habari Tanzania | Published  10/19/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Analis Mwandu, TSJ

MSHITAKIWA Salum Masudi (30) anayekabiliwa na kesi ya mauaji, jana alifanya vurugu katika Mahakama ya Wilaya ya Ilala kwa madai ya kutotendewa haki katika kesi hiyo.

Mshitakiwa huyo alifanya vurufu hizo baada ya Hakimu Mfawidhi wa mahakama hiyo, Mustafa Mlawa kuahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 30 kwa maelezo kuwa upelelezi wake haujakamilika.

Baada ya kutoka mahakamani, mshitakiwa huyo alipanda juu ya gari moja lililokuwapo mahakamani hapo huku akipiga kelele kuwa hatendewi haki, hivyo anataka kujinyonga.

Hali hiyo ilisababisha baadhi ya watu waliokuwapo mahakamani hapo kusubiri kesi zao kutajwa kutawanyika.

Kutokana na hali hiyo, askari waliokuwapo mahakamani hapo walimkamata na kumweka chini ya ulinzi, kisha akafunguliwa mashitaka ya kufanya fujo mahakamani.

Akisomewa mashitaka hayo na Mwendesha Mashitaka, Gervanus Muhume alidai kuwa jana, saa 4:00 asubuhi, alifanya vurugu katika mahakama hiyo, hivyo kusababisha kuvunjika kwa amani. Alikana tuhuma hizo na kesi itatajwa Oktoba 30


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.