SHIRIKA la Free Wheel Chair limetoa msaada wa baiskeli 550 kwa walemavu, zenye thamani ya sh 175,000,000, kupitia Kanisa la Christian Mission lililopo jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari katika Ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Askofu wa kanisa hilo, Mgullu Kilimba, alisema kanisa lao linatambua wajibu wake katika kushirikiana na serikali kuwaondolea Watanzania kero zinazosababishwa na ujinga, umaskini na maradhi.
Mgullu alisema wameandaa fomu maalumu kwa walengwa ambazo mlemavu atajaza na kuthibitishwa na viongozi wa kanisa na serikali za mita kuwa hana baiskeli.
Amewaomba wasamaria wema na serikali kwa ujumla kuchangia zoezi hilo, ili waweze kusambaza mikoani. Zoezi hilo litagharimu sh 15,000,000.