CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimeteua wagombea 38 watakaoingia katika mchakato wa kuwapata wagombea watakaogombea ubunge wa Afrika Mashariki.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Itikadi na Uenezi, Aggrey Mwanri, alisema majina hayo yaliteuliwa katika kikao cha Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM iliyokutana juzi chini ya Mwenyekiti wake, Rais Jakaya Kikwete.
Aliwataja walioteuliwa kwa upande wa Tanzania Bara ni Geogre Francis Nangale, Dk. Norman Adamson Siggala, Samwel Mwita Wangwe, Dk. Didas John Masaburi na Dk. Michael Onesmo Ndanshau.
Wengine ni Dk. Aman Kabourou, Dk. Baanda Ayub Salim, Evod Mmanda Herman, Dk. Handley Mpoki Mafwenga, Renatus Gervas Mkinga, Goodluck Joseph Ole-Madeye pamoja na Mwabani Rajabu Kambangwa.
Wagombea wengine ni Anamringi Issay Macha, Dk. Richard Simon Kassungu, Joseph Didas Kessy, Rogers Jacob Shemwelekwa, Gideon Kaino Mandes, Eliachim Jackson Simpasa, pamoja na Aloys Lusekelo Mwasongwe.
Kwa upande wa wanawake ni Kate Sylivia Kamba, Hulda Stenley Kibacha, Dk. Terezya Luoga Huvisa, Janet Deo Mmari, Rose Lilian Maeda, Janet Zebedeyo Mbene, Neema Massawe Nshumba, Hadija Kusola Kusaga na Eva Festo Makune.
Aliwataja wagombea kutoka Zanzibar kuwa ni Balozi Isaack Sepetu, Nassoro Juma Mugheir, Dk. Said Gharib Bilal, Abdallah Ali Hassan Mwinyi, Remedius Edington Kissassi, Dk. Yusuf Nuhu Pandu, Dk. Makame Ali Ussi na Rajabu Uweje Yakubu.
Kwa upande wa Zanzibar, wagombea wa kike ni wawili ambao ni Mahfoudha Alley Hamid na Sebtuu Mohamed Nassoro.
Pia kikao kiliwateua wanachama saba kuwa kaimu makatibu wa CCM mikoa na wengine 18 kuwa makatibu wa CCM wa wilaya. Uteuzi huo unatokana na kuwapo kwa nafasi za wazi katika mikoa na wilaya kwa sababu mbalimbali.
Aliwataja walioteuliwa kuwa kaimu makatibu wa mikoa ni, Mwangi Rajabu Kundya (Mwanza), Kilumbe Shaaban Ng’enda (Iringa), Verena Shumbusho (Rukwa), Mary Pius Chatanda (Morogoro), Asha Kipangula (Ruvuma), Stephen Mwale Kazidi (Lindi) na Mohamed Mbande (Arusha).
Alisema walioteuliwa kuwa makatibu wa CCM wilaya bado hawajapangiwa vituo vya kazi ambao ni Sauda Mpambalyoto, Richard Kaseja, Sikujua Athuman, Kassim Mabrouk Mbarak na Hadija Faraji.
Wengine ni Mohamed Seleman, George Yesaya Zakaria, Aziza Ramadhani Mapuri, Mberito Magova, Rahel Ndegeleke, Jamila Mjungu, Musa Homera, Saleh Said Kikweo, Sidael Goroi Langishe, Robert Kerenge, Mary Tesha, Rehema Khalifani na Subira Mohamed Ali.
Alisema kuwa Kamati Kuu pia ilielekeza kuanzishwa kwa Chuo cha CCM Ilehemi mkoani Iringa, ikiwa ni pamoja na kuandaliwa kwa mafunzo ya muda mfupi kwa makada na viongozi ili kuimarisha uwezo wa kiongozi kiutendaji, ikiwa ni pamoa na semina za maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa CCM 2007.