Na. Prosper Kwigize, Kibondo.
Wananchi wazaliwa wa wilaya ya Kibondo waliofanikiwa kufaulu masomo ya msingi na sekondari na hatimae kupata kazi katika mikoa mbalimbali wamepewa wito wa kukumbuka nyumbani na kushiriki kupaendeleza.
Wito huo umetolewa mwishoni mwa wiki na afisa elimu wilaya ya Kibondo Bi. Fides Mnyogwa wakati akihutubia mahafali ya darasa la saba katika shule ya msingi Kasanda wilayani humo.
Amesema inasikitisha sana wilaya kukosa watumishi hususani walimu kwa kisingizio cha mazingira magumu ya wilaya wakati wapo wazawa ambao wangeweza kuja kufanya kazi wilayani humo.
Bi. Mnyogwa amebainisha kuwa wha wengi wana kasumba ya kutotaka kufanya kazi kwao ndiko kunakochangia wilaya kutopata maendeleo na kukosa watumishi wa idara mbalimbali.
Aidha amewataka wanafunzi wanaomaliza elimu ya msdingi na sekondari weatakaofanikiwa kuendelea na elimu nyingine waone fahali kufanya kazi kwao badala ya kupakimbia na kuongeza kuwa Kigoma itajengwa na wana Kigoma.
Awali akimkaribisha afisa elimu kuhutubia waanchi, walimu na wanafunzi mwenyekiti wa kamati ya shule hiyo Bw. Mathias Kaura aliwahimiza wanafunzi kuwa makini hasa wale wanaoonekana kuingia utu uzima kwani gonjwa hatari la ukimwi ni moja ya vikwazo kwa vijana.
Amewahimiza kuwa na hamu zaidi ya kujisomea badala ya kukimbilia kuolewa au kufanya kitendo cha ngono ovyo ili malengo na ahadi walizojiwekea zitimie na kuwawezesha kuwa wakombozi wa kaya na koo zao.
Amewaonya pia vijana wa mtaani kutoona fahali kuwachukua wasichaa wadogo kimapenzi hususani wanafunzi na kuongeza kuwa tabia hiyo italimaliza taifa kutokana na kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya ukimwi.
Jumla ya wanafunzi 210 wamehitimu ya elimu ya msingi katika shule ya msingi Kasanda ambayo sasa imegawanywa kuwa shule mbili na kuzaliwa kwa shule mpya ya Tumaini