Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mahita amkana mtoto
Mahita amkana mtoto
By Habari Tanzania | Published  10/17/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Irene Mark

ALIYEKUWA Mkuu wa Jeshi la Polisi, Inspekta Jenerali (IGP), Omari Mahita, amemkana mtoto Juma Omari Mahita (8), anayedaiwa kuzaa na yaya wake, Rehema Shaabani.

Mahita, amemkana mtoto huyo kupitia utetezi wake aliowasilisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki kupitia kwa wakili wa kujitegemea, Charles Semigalawe.

Katika utetezi huo wa maandishi, Mahita ameieleza mahakama kwamba yeye si baba wa mtoto huyo.

Ameeleza kuwa madai ya mwanamke huyo kuwa Mahita, alikuwa Mkuu wa Polisi Mkoa (RPC) wa Kilimanjaro mwaka 1996, si ya kweli.

Utetezi huo umeeleza kwamba mlalamikaji alikuwa mtumishi wake wa ndani mwaka 1995, na hakuwa na mawasiliano naye baada ya kuacha kazi mwishoni mwa mwaka huo.

“Huyo Juma simtambui wala huyo mwanamke pia sina mawasiliano naye, tangu alipoacha kazi nyumbani kwangu mwaka 1995,” inasema sehemu ya utetezi huo.

Mahita, ameeleza kuwa mwaka 2003, akiwa IGP, mlalamikaji alifika nyumbani kwake Mtaa wa Bongoyo, Dar es Salaam na kufanya fujo akitaka Juma ahudumiwe.

Utetezi umeeleza kuwa, Mahita aliwaamuru askari wamfukuze mlalamikaji.

“Alipotoka kwangu alienda Ukonga nyumbani kwa dada yangu bila utambulisho wowote, alimwacha mtoto huyo… kwa huruma yangu niliamua kumpeleka mtoto huyo kwa Sheikh Yahaya Hussein ili ajifunze Kuran,” inasema sehemu ya utetezi huo.

Kesi hiyo namba 2/2006 ambayo ipo mbele ya Hakimu Mkazi, Pellagia Khaday, itasikilizwa leo.

Mahita anadaiwa kumtelekeza mtoto huyo. Mlalamikaji anaiomba mahakama imwamuru Mahita amlipe sh 100,000 kila mwezi kuanzia mwaka 1997, kama matunzo ya mtoto huyo hadi atakapohitimu shule.

Juma anasoma darasa la tatu katika Shule ya Msingi Muungano iliyopo Kinondoni, Dar es Salaam.

Maelezo ya mlalamikaji yanaonyesha kuwa uhusiano wa kimapenzi kati yao watu hao wawili ulianza Mei, 1996 hadi Oktoba, 1996.

Mlalamikaji anadai kwamba Mahita alimpa sh 40,000 na kushauriwa arudi nyumbani kwao Kondoa ili mkewe (ambaye sasa ni marehemu) asifahamu.

Mahita anadaiwa kufanya hivyo kwa ahadi kwamba angemlea mtoto atakeyezaliwa.

Katika kesi hiyo yenye mvuto kwa wakazi wa Dar es Salaam na vitongoji vyake, mlalamikaji anatetewa na Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC).


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by tausi omari)
    Rating
    too much repetition of the same story. the story is not telling us anything new and needs to ellaborated
     
  • Comment #2 (Posted by McFallan)
    Rating
    Dawa ya Longolongo ndogo. Kama mtoto si wa Mahita au wa Mahita; katika zama hizi za Sayansi na Teknolojia, mbona hili ni suala dogo tu. Mahita na Mtoto wakachukuliwe vipimo vya DNA na mchezo utakuwa umeeleweka. Inaumiza kwa sehemu, maana kama mtoto ni wa Mahita, kukana damu yake sio vema. Ila kama pia anasingiziwa, kutaka kujipatia umaarufu kwa kuwaweka watu wengine matatani sio vema pia.
     
  • Comment #3 (Posted by millanga ha)
    Rating
    kama mr Mahita hataki mtoto apime dna ikionyesha si wake wasamalia wema watamsaidia. Lakini asikwepe jukumu lake au sheria ichukue mkondo wake
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.