Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ajali zaua 17, majeruhi 77 Mbeya, Ruvuma
Ajali zaua 17, majeruhi 77 Mbeya, Ruvuma
By Habari Tanzania | Published  10/16/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Merali Chawe, Mbeya
WATU 17 wamekufa na wengine 77 kujeruhiwa katika ajali mbili tofauti zilizotokea mkoani Mbeya na Ruvuma jana na juzi baada ya basi na lori aina ya Fuso kupata ajali.

Katika ajali ya Mbeya abiria 11 wamekufa na wengine 25 kujeruhiwa wakiwa safarini kutoka Zambia kwenda jijini Dar es Salaam basi la Tawfiq lilipopinduka katika kijiji cha Machimbo wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya.

Kamanda wa Polisi wa mkoa Mbeya, Suleiman Kova, aliiasema jana kuwa ajali hiyo ilitokea saa 7:45 mchana baada ya gurudunu la kushoto kupasuka na kulifanya liache barabara na kugonga mti kabla ya kupinduka.

Alisema basi hilo baada ya kupasuka gurudumu dereva alijaribu kulirejesha barabarani lakini gurudumu la kulia pia ilipasuka na kulifanya linyumbe na kugonga mti.

Kamanda Kova aliwataja waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni madereva wawili wa basi hilo, Joseph Msuya (55) na Ngome Zakayo (54) wote wakazi wa Dar es Salaam.

Wengine ni Kondakta wa basi hilo, Joho (35) mkazi wa Tanga na utingo wawili, Juma Mwanga (25), na Zuber Athuman (30) wote wakazi wa Dar es Salaam.

Kamanda Kova aliwataja wengine kuwa ni abiria Doroith Mwalusaka (50-55) na Amon Mwalusaka (64) ambo ni raia wa Zambia. Abiria mwingine Mika Mwengela hajafahamika miaka yake na wengine watatu bado hawajafahamika majina yao.

Alisema majeruhi 22 walipelekwa kutibiwa katika hospitali ya Chimala na watatu walipelekwa katika hospitali ya Ilembula.

Kutoka Songea, Joyce Joliga, anaripoti kuwa watu sita wamefariki dunia katika ajali ya gari na wengine 52 wamelazwa katika hospitali ya wilaya ya Tunduru baada ya kujeruhiwa vibaya shemu za miili yao katika ajari iliyotokea nje kidogo ya Wilaya ya Tunduru,mkoani Ruvuma.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ruvuma,Falhum Mshana ameliamba Mwananchi kuwa ajali hiyo imetokea juzi saa 12:20 jioni katika bara bara ya Tunduru kijiji cha Sevuyanga baada ya gari aina ya Fusso Mistubishi lililokuwa likitokea Tunduru kwenda Masasi, kuacha njia na kupinduka.

Kamanda Mshana, amewataja waliokufa katika ajari hiyo kuwa ni Issa Omary (24) mkazi wa Tinginya na Asia Chombo (3) mkazi wa Karanji wilayani Tunduru ambao tayari miili yao imeshatambuliwa na jamaa zao, wengine ni wanawake wawili na wanaume wawili ambao bado awajatambuliwa.

Alisema mara baada ya ajali hiyo dereva wa gari hiyo alitoroka na chanzo cha ajali hiyo kimeelezwa kuwa kimetokana na mwendo mkali pamoja na mizigo mingi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.