Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ashtushwa na wanaotaka kumsomea ‘albadir’ Mengi
Ashtushwa na wanaotaka kumsomea ‘albadir’ Mengi
By Habari Tanzania | Published  05/27/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
l Ni Sheikh Bassaleh wa Msikiti wa Mtoro
 
Na Mwandishi Wetu
 
KIONGOZI wa dini ya Kiislamu katika Msikiti wa Idrisa jijini Dar es Salaam, Sheikh Ali Bassaleh, amesema ameshtushwa na taarifa zilizoandikwa na gazeti moja la kila wiki juu ya waumini wa Msikiti huo kumsomea 'albadir' Menyekiti Mtendaji wa IPP, Reginald Mengi.
 
Sheikh Bassaleh alisema jana kuwa taarifa hizo ni potofu, mbaya na kwamba kitendo hicho si cha kuchukuliwa kwa pupa kwa vile kina madhara makubwa kwa mtu anayekusudiwa kufanyiwa hivyo.
 
Alisema hatua ya mtu kusomewa duwa hiyo huwa ni ya mwisho na kuonya kuwa wenye nia ya kufanya hivyo hawana budi kuacha mara moja kwa vile inaweza kumwathiri mhusika na watu wanaomtegemea.
 
Kutokana na hali hiyo, alisema waumini wa dini ya Kiislamu ambao wamepania kufanya hivyo wawe na subira na kwamba duwa hiyo ni hatua ya mwisho katika kunuia kufanya jambo lolote.
 
"Wale ambao wanaelewa mambo haya wanafahamu kuwa duwa maalum ya albadir haina kinga na inawateketeza maskini na wafalme. Nafsi yangu imenisuta na kunitaka nijitahidi kumuokoa binadamu mwenzangu katika janga lililo mbele yake," alisema.
 
Alisema madhara ya kusomewa kwa duwa hiyo siyo kwamba yatamkumba Mengi pekee, bali familia yake na wafanyakazi aliyowaajiri katika kampuni mbalimbali anazozimiliki.
 
Kutokana na hali hiyo, kiongozi huyo wa kidini amewasihi waumini wa Kiislamu walionuia kufanya hivyo kutafakari kwa undani athari za jambo hilo.
 
Gazeti moja la kila wiki juzi katika toleo lake la Mei 25 hadi 31, liliandika habari juu ya waumini wa Msikiti wa Idrisa kumsomea dua ya albadir Mengi kwa madai kuwa amewakashifu Waislamu na kutishia kumfikisha mahakamani Sheikh Bassaleh.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.