Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Rais apangua wizara nne
Rais apangua wizara nne
By Habari Tanzania | Published  10/16/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Mwandishi wetu
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko makubwa katika baraza lake la mawaziri kwa kuwahamisha vituo vya kazi mawaziri 10 na naibu mawaziri wanane.

Katika mabadiliko hayo wizara ya Nishati na Madini, Mambo ya Ndani ya Nchi, Viwanda na Biashara, Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana mawaziri wake wote wamehamishiwa wizara nyingine.

Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika waziri na naibu waziri mmoja nao wamehamishiwa katika wizara nyingine.

Wizara nyingine zilizohamishwa waziri au naibu waziri mmoja ni Wizara ya Maliasili na Utalii, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Miundombinu, Maendeleo ya Mifugo na Maji, Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto na Mipango, Uchumi na Uwezeshaji.

Kwa mujibu wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana, mawaziri waliohusika na mabadiliko hayo na wizara zao za zamani kwenye mabano, ni Anthony Diallo (Maliasili na Utalii) ambaye amehamishiwa katika Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Profesa Jumanne Maghembe (Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana) anayekwenda katika Wizara ya Maliasili na Utalii.

Wengine, ni Dk Ibrahim Msabaha (Nishati na Madini) anayehamia Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Nazir Karamagi (Viwanda na Biashara) anayekwenda Wizara ya Nishati na Madini, Basil Mramba (Miundombinu) aliyehamishiwa Viwanda na Biashara na Kapteni John Chiligati (Mambo ya Ndani) aliyehamishiwa katika Wizara Kazi, Ajira na Vijana.

Mawaziri wengine, ni Andrew Chenge (Ushirikiano Afrika Mashariki) aliyehamishiwa katika Wizara ya Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa (Maendeleo ya Mifugo) aliyehamishiwa Wizara ya Maji, Stephen Wassira (Maji) aliyehamishiwa katika Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Joseph Mungai (Kilimo, Chakula na Ushirika) aliyehamishiwa katika Wizara ya Mambo ya Ndani.

Naibu Mawaziri waliohamishwa wizara zao na kupelekwa wizara nyingine, ni Dk Emmanuel Nchimbi (Habari, Michezo na Utamaduni) anayekwenda Wizara ya Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Daniel Nsanzugwanko (Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana) anayehamia Wizara ya Habari, Michezo na Utamaduni, David Mathayo (Biashara na Viwanda) anayekwenda Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na Hezekiah Chibulunje (Kilimo, Chakula na Ushirika) anayehamia Wizara ya Viwanda na Biashara.

Wengine ni Dk Batilda Buriani (Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto) anayekwenda katika Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji, Salome Mbatia (Mipango, Uchumi na Uwezeshaji) anayehamia Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Lawrence Masha (Nishati na Madini) anayekwenda Wizara ya Mambo ya Ndani na Bernard Membe (Mambo ya Ndani) anayekwenda Wizara ya Nishati na Madini.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mwandishi wa Habari Msaidizi wa Rais, Maura Mwingira, ilieleza kuwa mawaziri na manaibu mawaziri hao, wataapishwa leo na Rais Kikwete saa 9:00 alasiri Ikulu, jijini Dar es Salaam.

Hii ni mara ya kwanza kwa Rais Kikwete kufanya mabadiliko ya baraza lake la mawaziri tangu aingie madarakani Novemba mwaka jana.

Ingawa taarifa ya Ikulu haijaeleza sababu za mabadiliko hayo , lakini ni kutaka kuimarisha safu yake ya uongozi baada ya kuongoza kwa karibu mwaka mmoja.

Wakati akitangaza baraza lake la mawaziri, Rais Kikwete alisema muundo wa serikali ya awamu ya nne umetegemea ajenda na majukumu yaliyopo katika kipindi cha miaka mitano cha uongozi wa serikali hiyo.

Alisema licha ya majukumu na ajenda pia baraza lake limelenga katika kushirikisha uwakilishi wa jamii mbalimbali.

Rais Kikwete alisema amefanyia marekebisho baadhi ya wizara kwa kuzipunguzia majukumu na kuunda wizara mpya kwa ajili ya kutekeleza ajenda zilizopo.

Alisema serikali mpya ina mambo mapya ambapo wengi wa mawaziri na naibu mawaziri aliowateuwa ni wapya, na kuongeza kuwa mawaziri wa zamani ambao hawakuchaguliwa, uzoefu wao utatumika na siyo kwamba walishindwa kazi ila haiwezekani kurejesha baraza lote la Rais Mkapa.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.