Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kamati Kuu CCM kukutana kesho
Kamati Kuu CCM kukutana kesho
By Habari Tanzania | Published  10/15/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

KAMATI Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), inatarajiwa kukutana kesho chini ya Mwenyekiti, Rais Jakaya Kikwete.

Taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mwenezi wa CCM, Aggrey Mwanri, inaeleza kuwa kikao hicho cha siku moja kimetanguliwa na kikao cha siku mbili cha Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa, ambacho ndicho kilichoandaa agenda ya Kamati Kuu.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa agenda zilizowasilishwa kwa Kamati Kuu na Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa ni pamoja na maandalizi ya uchaguzi mkuu wa CCM ambao utafanyika mwakani, kuanzia ngazi ya shina hadi taifa, uandaaji na uchaguzi katika mashina ya CCM nje ya nchi.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Kamati Kuu pia itapokea mapendekezo ya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kuhusu wanachama wa CCM wanaoomba kuteuliwa kugombea ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki.

Jumla ya wanachama wa CCM 49 kutoka nchi nzima wamejitokeza kuomba wateuliwe kugombea nafasi nane kati ya tisa zilizotengwa kwa Tanzania Bara katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Chama Cha Mapinduzi kina nafasi nane na upinzani ni moja, kutokana na uwiano wa idadi ya wabunge ndani ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Miongoni mwa wabunge wanane watakaochaguliwa na wabunge wote wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuingia katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa tiketi ya CCM, watano watakuwa wanaume na watatu ni wanawake


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.