Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Msafara wa Waziri Mkuu wakwama
Msafara wa Waziri Mkuu wakwama
By Habari Tanzania | Published  10/13/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na James Marenga, Kilindi

MSAFARA wa Waziri Mkuu, Edward Lowassa, umekwama wilayani Kilindi ulipokuwa ukienda kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa ufanyike katika Tarafa ya Kimbe.

Msafara huo ulilazimika kuishia katika Kijiji cha Legero, maili 25 kuelekea katika tarafa hiyo.

Kukwama huko kumetokana na ubovu wa barabara kutoka Morogoro hadi Handeni yenye urefu wa kilometa 70.

Mkuu wa Wilaya ya Kilindi, Sarah Dumba, alilazamika kwenda kuitwa kutoka Kimbe ambako alikuwa amewakusanya wananchi kwa ajili ya kusubiri mkutano huo.

Miongoni mwa viongozi waliokuwamo kwenye msafara huo ambao walishuhudia adha hiyo ni Naibu Waziri wa Miundombinu, Dk. Milton Mahanga.

Akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Legero, Waziri Mkuu alikemea tabia ya baadhi ya wakzi wa Handeni kuuza mazao yao kwa bei rahisi, kisha baadaye kuuziwa mazao hayo kwa bei ya juu.

Alitoa mfano kuwa wanauza mahindi kwa sh 12,000 kwa gunia, baada ya msimu wanauziwa mahindi hayo kwa sh 35,000 kutokana na kutokuwa na akiba ya chakula. Aliwahimiza kuhifadhi chakula.

Hata hivyo, mkutano huo ulifanyika bila kuwapo kwa mkuu wa wilaya wa eneo hilo, kwani alikuwa Kimbe, ambako awali mkutano huo ulipangwa kufanyika.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.