Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Waliomteka mtoto wazidisha vituko
Waliomteka mtoto wazidisha vituko
By Habari Tanzania | Published  05/14/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Wateka nyara wa mtoto Humudy Aboubakary (3) pichani mkazi wa Magomeni Makurumla na Uweje, jijini Dar es Salaam ambao bado wanaendelea kumshikilia mtoto huyo, sasa wamempiga picha na kisha kuzituma kwa wazazi wake wakisisitiza kutaka sh milioni 5 ili kumtoa mtoto huyo.

Akizungumza na Nipashe jana, mama mdogo wa mtoto huyo Bi.Hadija Lumbu alisema picha hizo pamoja na barua ya kuwataka kuendelea kutuma fedha hizo kwa wateka nyara hao zilitumwa kwao Mei 8 mwaka huu.

Akielezea zaidi alisema njia iliyotumika kutuma picha hizo alisema: ’’Tulikuwa ndani tumekaa tukasikia mtu akigonga mlango, ndipo tukaenda kufungua, kaka mmoja muuza mayai akatuambia ’kaka yenu kasema chukueni mayai trei mbili pamoja na hii barua... kasema yeye anawahi kazini’. Sisi baada ya kuchukua bahasha hatukuchukua tena mayai,’’.

’’Tulipomuhoji zaidi muuza mayai huyo alisema kuwa akiwa anauza mayai alipita katika nyumba yetu na kukuta nje kukiwa na gari nyeupe imepaki ndipo kaka mmoja akamuita yeye na kumwambie kuwa agonge katika geti letu na atakayetoka amwambia kuwa kaka yao amewaambia wachukue mayai trei mbili na atupe barua, na yule muuza mayai kwa kweli hakufahamu kinachoendelea,’’ alisema.

Alisema katika barua hiyo walikuta picha tatu zilizokuwa zikimuonyesha mtoto huyo akiwa katika pozi tofauti, ambapo picha ya kwanza ilimuonyesha akiwa amelala kitandani, ya pili akiwa amekaa kwenye kiti na nyingine akiwa kasimama nje ya mlango na pia macho ya mtoto huyo yakionyesha kuvimba kama mtu aliyekuwa akilia kwa muda mrefu.

Pia katika barua iliyotumwa kwao iliendelea kusisitiza kuzitaka pesa zao ili waweze kumuachia mtoto huyo ambapo walidai kuwa amewachosha.

Pia watekaji hao walieleza katika barua hiyo kuwa juhudi za wanafamilia hiyo kukimbilia polisi, ITV au kwenye magazeti ni kazi bure na wanachotaka ni pesa tu.

’’Walituambia kwenye barua hiyo kuwa masharti yetu ya kwanza mnayafahamu, nashangaa hamyafuati mnang’ang’ana na waandishi wa habari na mapolisi, haiwasaidii kitu sisi tunataka fedha tu, na tutumieni vocha kwenye simu tuliyowapa na mtoto wenu mtamkuta kwenye hoteli yoyote ile,’’ alisema.

Bi Lumbu alisema mpaka sasa tayari wameshatuma vocha za simu zenye thamani ya sh lako tano(Sh.500,000/-) kwenye simu waliyoelezwa.

Leo Jumapili ni siku ya 17 tangu mtoto huyo aibiwe na msichana wa kazi aliyetambulika kwa jina moja la Mwanaheri mwenye umri kati ya miaka 24 na 25.

Mama wa mtoto huyo, Bi. Ng’ase Lumbu yupo katika hali mbaya kwani kila anapokuwa akimbuka mtoto wake au akisikia watu wakizungumza amekuwa akilia.

Hali hiyo ya kulia imekuwa ikimfanya mama huyo kuumwa mara kwa mara na kulazimika kunywa dawa na hata Nipashe Jumapili ilipokuwa ikifanya mazungumzo naye alikuwa akilia na baadaye kushindwa kuendelea kuzungumza.

Awali mama wa mtoto huyo Bi Ng’ase Lumbu alisema mtoto huyo aliibiwa Aprili 27 mwaka huu majira ya saa 10:00 jioni .

Bi. Nga’se alieleza kuwa baada ya mwanae kuibwa alimtafuta usiku kucha lakini juhudi zake ziligonga mwamba.

Hata hivyo alisema majira ya asubuhi siku iliyofuata alikuta karatasi imetupwa pembeni mwa nyumba na alipoifungua ilikuwa na namba ya simu na maandishi yaliyomtaka kuwapigia simu watu waliomchukua mtoto wake.

’’Nilipopiga namba hiyo ya simu, watu waliopokea walikuwa ni wanaume ndipo waliponiambia kuwa mtoto wangu wanae na wanataka niwape Sh. milioni tano na kwa kuanzia nianze kutuma vocha ya simu ya Dola 50 na endapo nisipofanya hivyo wataondoka nchini na mtoto wangu,’’ alisema mama huyo huku akilia.

Alisema tayari wamesharipoti tukio hilo polisi na kupata namba ya faili, MAG/RB/10109/06.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Bw. Alfred Tibaigana hakupatikana kuzungumzia suala hilo jana.
  • SOURCE: Nipashe

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.