WAZIRI Mkuu, Edward Lowassa, amewataka wananchi wa Tanga kutokubali kutapeliwa na wawekezaji na kuwauzia viwanja kwa bei nafuu.
Alisema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara mjini hapa.
Alisema wawekezaji wanaweza kutumia ujanja wa kupata viwanja kwa bei chee. “Wawekezaji hawa wa sekta ya utalii wanaweza kuwarubuni mkauza kiwanja cha sh milioni 20 kwa sh milioni 10,” alisema.
Waziri Mkuu alisema wananachopaswa kufanya ni kuwahusisha maofisa ardhi.
Alisema sekta ya utalii inakua kwa kasi wilayani humo, mwananchi anachotakiwa ni kuchangamkia kwa kuingia nao ubia au kuchangamkia ajira zitakazotokana na sekta hiyo.
Wilaya ya Pangani ni moja ya wilaya zenye historia ya mambo ya kale, ikiwamo biashara ya utumwa. Akiwa wilayani hapo alitoa sh milioni tatu kutunisha mfuko wa vyama vya kuweka na kukopa (SACCOS) za kina mama za Jitegemee, Mshikamano na ya Wakulima, na mke wa Waziri Mkuu, Regina Lowassa, alitoa sh milioni moja