Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mbunge achangia ujenzi wa sekondari
Mbunge achangia ujenzi wa sekondari
By Habari Tanzania | Published  10/9/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Steven William, Muheza

MBUNGE wa Muheza, Hebert Mtangi, ameahidi kutoa mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ambayo inatarajiwa kujengwa katika Kijiji cha Mwembeni, Kata ya Magoroto wilayani hapa.

Mtangi alitoa ahadi hiyo juzi alipofanya ziara yake ya siku moja ya kuwashukuru wananchi wa kijiji hicho kwa kumchagua pamoja na kuhamasisha maendeleo katika jimbo hili.

Alisema ameamua kufanya hivyo kwa sababu kata hiyo haina shule ya sekondari, kitu ambacho kinafanya wanafunzi ambao wanamaliza elimu ya msingi kupata tabu ya kwenda kusoma shule za mbali.

Mbunge huyo aliwataka wananchi wa kata hiyo kujitolea nguvu zao katika ujenzi wa sekondari hiyo ili umalizike mara moja, na wanafunzi watakaofaulu waweze kujiunga katika sekondari hiyo.

Wananchi hao walimhakikishia mbunge huyo kuwa wapo tayari kuchangia kufanikisha ujenzi huo, lakini wamechoka, kwa kuwa awali uongozi wa kijiji hicho uliwachangisha fedha kwa ajili ya ujenzi wa sekondari hiyo, lakini fedha hizo zilitafunwa.

Kwa upande wake, mbunge huyo aliwashauri wananchi hao kutokata tamaa na kuendelea kuchanga kwa ajili ya ujenzi wa sekondari hiyo, na kwamba kiongozi yeyote atakayekula fedha za wananchi atachukuliwa hatua kali za kisheria


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.