Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Kandoro aunda tume kuchunguza ufisadi
Kandoro aunda tume kuchunguza ufisadi
By Habari Tanzania | Published  10/9/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Asha Bani

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Abbas Kandoro, amesema ameunda tume ya kuchunguza ufisadi unaofanywa na wafanyabiashara wakubwa ambao wanawatumia wafanyabiashara wadogo wadogo (wamachinga) kwa lengo la kukwepa kodi.

Alisema jana kuwa, uchunguzi uliofanywa na baadhi ya watendaji wa serikalini, umebaini kuwa wamachinga waliokuwa wamezagaa katika mitaa mbalimbali ya jiji, ukiwamo Mtaa wa Kongo, walikuwa wakitumiwa na baadhi ya wafanyabiashara wenye mitaji mikubwa kwa lengo la kukwepa kodi.

Kandoro alisema endapo mfanyabiashara yeyote atabainika kufanya kitendo hicho, atachukuliwa sheria kali kwa kuwa atakuwa ameiibia serikali kwa kukwepa kodi.

“Wamachinga wengi ambao walikuwa wanafanya fujo, na ambao walikuwa hawataki kutulia katika maeneo, ni wale ambao walikuwa wanatoa bidhaa katika maduka ya wakubwa,” alisema Kandoro.

Aliwasihi wafanyabiashara hao kukaa katika maeneo yao waliyopangiwa, ili waweze kusaidiwa hata kwa kupatiwa mikopo wakiwa katika vikundi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.