Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Magari ya mawaziri yaleta kizaazaa Z’bar
Magari ya mawaziri yaleta kizaazaa Z’bar
By Habari Tanzania | Published  10/8/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Mwandishi Wetu

MAGARI matatu ya mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), yamesababisha mtafaruku mkubwa, baada ya gari la Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, Sherry Khamis kukamatwa kisha magari hayo kuachiwa na maofisa wa Baraza la Manispaa.

Mzozo huo umekuja baada maofisa hao kukamata gari la mwenyekiti huyo na kulifunga matairi yake kwa minyonyoro, kwa madai kwamba liliegeshwa katika maeneo yasiyoruhusiwa kisheria.

Wakati gari hilo likifungwa minyonyoro mbele ya Soko Kuu la Zanzibar eneo la Darajani, kulikuwa na magari mengine katika eneo hilo hilo, likiwamo la Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi, Adam Mwakanjuki; Waziri wa Nchi Afisi ya Waziri Kiongozi, Amina Salum Ali; Waziri wa Kilimo, Maliasili na Mazingira, Burhani Saadat na la Mkuu wa Kikosi cha Valantia.

Magari hayo yaliachwa kama yalivyo, licha ya kuwa yameegeshwa katika maeneo hayo kinyume cha sheria, jambo ambalo lilisababisha mtafaruku mkubwa kati ya maofisa hao na wananchi katika eneo hilo.

“Kwa nini gari yangu mnaifunga minyonyoro wakati kuna magari mengi katika eneo hili na hamjachukua hatua yoyote?” alihoji Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Zanzibar, Sherry Khamis.

Gari ya kiongozi huyo, aina ya Toyota yenye namba ZNZ 30215, ilikamatwa mwendo wa saa 4 asubuhi, likafungwa minyororo, na hadi saa 5 lilikuwa halijafunguliwa minyonyoro hiyo.

Hata hivyo, maofisa wa Baraza la Manispaa waliokuwapo wakati wa tukio hilo, walisema kwa mujibu wa sheria ya maegesho, magari ya viongozi wa kitaifa hayatakiwi kufungwa minyonyoro, hata kama yameegeshwa kinyume cha sheria.

“Kwa mujibu wa sheria na maelekezo tuliyopewa na viongozi wetu, magari ya viongozi hayapaswi kufungwa minyororo, hata yakibainika yameegeshwa kinyume cha sheria,” alisema ofisa mmoja wa baraza hilo.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Usafirishaji katika Baraza la Manispaa, Ali Kombo, alisema maofisa wa manispaa waliitafasiri vibaya sheria, kwa vile magari yote yanayoegeshwa katika maeneo yasiyoruhusiwa, yakiwamo ya viongozi wa kitaifa, yanapaswa kuchukuliwa hatua.

Alisema kwamba, kwa mujibu wa sheria ya maegesho, gari yoyote inayoegeshwa katika eneo lisiloruhusiwa, inatakiwa ikamatwe, na iwapo mhusika atapatikana na hatia, faini yake ni sh 30,000 pamoja na gharama za utunzaji gari; sh 60,000.

“Sheria haibagui waziri au mkurugenzi, tunatunga sheria kwa ajili ya kutumika kwa wananchi wote, lakini tuna tatizo la kutokuwa na minyororo ya kutosha ya kuyafunga magari yote kwa wakati mmoja,” alisema Kombo.

Hata hivyo, gari la Mwenyekiti wa Baraza la Michezo liliachiwa baada ya kulipa sh 5,000, japokuwa iwapo angepelekwa mahakamani angelazimika kulipa sh 30,000 na gharama za usumbufu.

Tangu Baraza la Manispaa lianze kuyafunga magari yanayokiuka sheria za maegesho, kumejitokeza malalamiko mengi kuwa zoezi hilo linatawaliwa na ubaguzi, kwa vile magari yanayofungwa ni ya wananchi wa kawaida, lakini yale ya serikali, yakiwamo ya mawaziri huachiwa kuvunja sheria


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by ackah)
    Rating
    I am uphold by the lack of knowledge of the people working in the government. Employees need to know their jobs before hand. Where is the democracy when we are being treated differently from the people in the higher power. Kudoz to sharifa khamis for trying to correct the system.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.