Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Bilioni 5 kujenga bustani ya Nyerere
Bilioni 5 kujenga bustani ya Nyerere
By Habari Tanzania | Published  10/8/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Shabani Matutu

SERIKALI imepanga kujenga bustani ya kumbukumbu ya kumuenzi Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, itakayogharimu jumla ya dola mil 4 (zaidi ya sh bilioni 5).

Bustani hiyo inatarajia kujengwa mbele ya kiwanja cha wazi kilicho mbele ya nyumba yake, kiwanja ambacho kilikuwa kimevamiwa na mfanyabiashara aliyeweka makontena na kufyatua matofali.

Habari kutoka Taasisi ya Mwalimu Nyerere (MNH), zinasema kwamba kibanda cha kioo kilichotumika wakati wa kutoa heshima za mwisho kwa mwili wa Mwalimu baada ya kifo chake kilichotokea Hospitali ya St. Thomas, Uingereza, kitawekwa katika bustani hiyo.

Mradi huo umetambulishwa kama Ustawishaji wa Bustani ya Kumbukumbu ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius K. Nyerere, au Mwalimu Nyerere Memorial Park, na umelenga kwa ajili ya Watanzania wote na wapenda amani kote ulimwenguni.

Katika bustani hiyo kutakuwa na maktaba ambayo itawekwa vitabu vya Mwalimu Nyerere, magazeti na vitu vyake vya kihistoria, pia kutakuwa na mgahawa kwa ajili ya wageni.

Bustani hiyo itakuwa na vikundi vya burudani asilia vitakavyokuwa vikitoa burudani ya ngoma za asili na burudani hiyo itakuwa katika mahadhi ya Kiafrika, Kiasia na Ulaya.

Katika bustani hiyo kutakuwa na kiwanja cha michezo ya mpira wa miguu kwa watoto na watu wazima, na pia kutakuwa na mchezo wa bao katika kibanda cha asili cha msonge. Mwalimu alikuwa mchezaji na mpenzi mkubwa wa mchezo wa bao.

Mradi huo utatekelezwa katika hatua mbili. Hatua ya kwanza itakayogharimu dola 272,000 (sh zaidi ya milioni 354) imepangwa kuanza Septemba 2006 hadi Machi 2007. Hatua ya pili ya mradi huo imepangwa kuanza Januari 2007 na itagharimu dola 250,000 (sh zaidi mil 325).

Wahandisi wanaohusika na mpango huo ni TMK Contractors Ltd iliyopo Manispaa ya Kinondoni, jijini Dar es Salaam. Wahamasishaji wa mradi huo ni Taasisi ya Mwalimu Nyerere na unasimamiwa na serikali yenyewe.

Mwalimu Nyerere alifariki mwaka 1999 akiwa na umri wa miaka 77, na kila mwaka Oktoba 14 huwa Siku ya Baba wa Taifa, ambayo huadhimishwa kitaifa kwa mapumziko na kufanya shughuli za kumkumbuka.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by wankyo)
    Rating
    Kilichonistusha kwanza ndugu mwandishi ni kiasi cha fedha ulichoeleza mwanzo... bilioni tano kujenga bustani.... hiyo ni bustani ya Abunuwasi au.....
    Halafu jumla ya fedha ulizoorodhesha katika ya hatua ya kwanza na ya pili ni dola 522,000 sasa hizo dola milioni 3.478 zimepotelea wapi. Mana mpaka sasa nashindwa kuelewa kama kosa liko katika uandishi au ndiyo habari zenyewe zilivyotoka MNF.
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.