Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  WILAYA YA KIBONDO NAYO YAPINGA BURUNDI NA RWANDA KUINGIZWA AFRIKA MASHARIKI
WILAYA YA KIBONDO NAYO YAPINGA BURUNDI NA RWANDA KUINGIZWA AFRIKA MASHARIKI
By Habari Tanzania | Published  10/7/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Kibondo
 
 WANANCHI wa kada mbalimbali wilayani Kibondo, wameungana na wenzao kadhaa katika mikoa Mara, Mwanza na Kagera, kupinga maombi ya nchi za Rwanda na Burundi kupewa uanachama katika Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC).
 
 Wakizungumza na Naibu Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Diodorus Kamala jana, wananchi hao wamepinga wazi wazo lolote la kuzikaribisha nchi hizo katika EAC.
 
 Moja ya sababu za kukataa kupokelewa kwa nchi za Rwanda na Burundi katika jumuiya hiyo ni pamoja machafuko ya kisiasa, ukabila na vita katika nchi hizo.
 
 Aidha wananchi hao wameshauri Burundi na Rwanda wapewe masharti, ikiwa ni pamoja na kusalimisha silaha zilizozagaa mikononi mwa wananchi ambazo zimedaiwa kuhusika katika uharifu mwingi nchini.
 
 Kwa upande wake jeshi la polisi wilayani Kibondo limeiomba serikali licha ya ushirikiano wa kijeshi na nchi za afrika mashariki Polisi nao wapewe fursa ya ushirikiano wa kipolisi na nchi hizo ili kupunguza uharifu unaofanyika mipakani.
 
 Kamanda wa polisi wilaya ya Kibondo SSP Twaha Ramadhan amemwambia naibu waziri kuwa jeshi la polisi Tanzania limekuwa likifanya kazi kubwa na ngumu ya kuzuia uharifu katika mipaka bila kupata ushirikiano mkubwa toka kwa polisi wan chi jirani.
 
 Dk. Kamala yuko katika ziara ya mikoa kadhaa akitangaza na kufafanua kazi za wizara hiyo ambayo ni mpya; kueleza fursa ambazo Watanzania wanaweza kuzipata kutoka EAC, na kukusanya maoni ya wananchi kuhusu Rwanda na Burundi kupewa uanachama EAC na muundo wa Shirikisho la Afrika Mashariki.
 
 Oktoba 13, mwaka huu, Rais Jakaya Kikwete, atatangaza Kamati maalumu ya kukusanya maoni ya wananchi katika wilaya zote nchini kuhusu Rwanda na Burundi kupewa uanachama, na pia muundo wa Shirikisho

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.