Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wenye viwanda vidogo Dar kuporomosha ghorofa
Wenye viwanda vidogo Dar kuporomosha ghorofa
By Habari Tanzania | Published  10/7/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Baada ya kusota kwa muda mrefu bila kuwa na ofisi, hatimaye ushirika wa viwanda vidogo Jijini Dar es salaam, DASICO hivi karibuni wanatarajia kujenga jengo la ghorofa nne litakalogharimu kiasi cha sh. bilioni 1 na milioni 425, ukiwa ni mpango wa maendeleo wa ushirika huo.

Akizungumza katika mkutano mkuu wa DASICO, Mwenyekiti wake Bw. Mfaume Yusufu, amesema tayari wameshaandaa michoro ya ramani ya jengo hilo na na hivi sasa wanasaka wawekezaji baada ya kupata ridhaa ya wanachama.

”Huo ni mpango mmojawapo wa maendeleo kati ya kadhaa tuliyojipangia. Tumeamua kuuleta kwenu kisha tutafute wawekezaji baada ya kupata ridhaa yenu wanachama kabla ya kuendelea na hatua nyingine,” amesema Bw. Yusuf.

Bw. Mfaume amesema ushirika huo una mipango mingi ya maendeleo na wataendelea kupiga hatua moja baada ya nyingine ili ushirika wao uweze kufanikiwa.

Akizungumzia upande wa ushirika wa kuweka na kukopa SACCOS, Mwenyekiti huyo amesema wamefanikiwa kuanzisha ushirika huo wa kuweka na kukopa na hivi sasa tayari wamepata usajili wa kudumu.

”Hata uanzishwaji wa Saccos ni mpango wetu mwingine wa kimaendeleo.

Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa huku mambo mengine tukitarajia kuyakamilisha baadaye, kwanini tushindwe?” akasema Mwenyekiti huyo

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.