Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Machinga wapiga bao la kisigino
Machinga wapiga bao la kisigino
By Habari Tanzania | Published  10/7/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Wafanyakazi ndogo ndogo maarufu kama Machinga
waliotimuliwa toka katika maeneo mbalimbali yasiyoruhusiwa kwa biashara zao Jijini Dar inadaiwa wameibuka na staili nyingine ya kuendesha biashara zao kwa raha katika maeneo yaleyale ambayo wametakiwa kuyahama.

Mbinu yenyewe ambayo sasa inaelekea kufunika jitihada zinazoendelea kufanywa katika kuwahamisha kwa operesheni kali zinazohusisha vikosi vya Mgambo wa Jiji na Askari Polisi, ni ile ya kuibukia maeneo husika nyakati za usiku.

Katika baadhi ya maeneo, Wamachinga hao wameonekana wakiibukia kwenye maeneo waIiyoondolewa nyakati za usiku na kisha kupanga bidhaa zao kabla ya kuendelea na biashara kama kawaida.

Hata hivyo, janja hiyo ya nyani ’imeshabumbuluka’ ambapo sasa, Manispaa ya Kinondoni imepiga marufuku tabia hiyo kupitia tangazo lake maalum kwa Wamachinga.

”... wapo wenye nyumba kwenye maeneo husika wanaoendelea kuhifadhi bidhaa za watu hao (machinga) mitaani kwa lengo la kuendelea na biashara hizo wakati wa usiku.

Manispaa inawaonya wote wafanyabiashara na wenye nyumba wanaowaficha wafanyabiashara hao, wakikamatwa watafikishwa Mahakamani kwa mujibu wa Sheria ya Biashara Na. 25 ya mwaka 1972...” imesema sehemu ya tangazo hilo la Manispaa ya Kinondoni.

Ili kutekeleza azma hiyo imesema wapo ’vijana wa kazi’ waliopangiwa zamu za kuzunguka mitaani nyakati za usiku ili kuwadhibiti Wamachinga wanaorejea kwenye maeneo yasiyoruhusiwa kibiashara.

Askari hao wa Jiji watakuwa wakipiga ’misele’ usiku sambamba na Askari Polisi watakaokuwa doria na imeelezwa na Manispaa kuwa atakayedakwa hatasalimika.

Tayari katika mitaa kadhaa ya Jiji, ’vijana wa kazi’ wa manispaa wameshaonekana wakiranda nyakati za usiku wakiwasaka Wamachinga wanaorejea kwenye maeneo yao ya zamani yasiyoruhusiwa kwa biashara.

Wakizungumza na Alasiri, baadhi ya wafanyabiashara wamesema kwamba kitendo cha wao kurudi kwenye maeneo hayo nyakati za usiku kinatokana na sababu kuwa wamekosa la kufanya hasa baada ya biashara zao kuyumbishwa na operesheni hiyo ya kuwaondoa .

Uchunguzi uliofanywa juzi katika maeneo kadhaa yaliyokumbwa na operesheni hiyo ya safisha Jiji, umeonyesha kuwa kila giza linapokaribia kuingia na mgambo wa Jiji kuondoka kwenye ’saiti’ zao, Machinga hufika kinyemela na kuendelea na biashara zao.

Kinondoni Morocco, Mwananyamala, Kituo cha mabasi Magomeni, Kituo cha mabasi kinachoendelea kujengwa Mwenge ni baadhi ya maeneo ambayo Machinga huonekana wakiyanyatia usiku na kuendelea na biashara zao.

Hata hivyo wakati mwingine hufanya hivyo kwa kujificha, wakihofu kunaswa na ’vijana wa kazi’ toka manispaa

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.