Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  TTCL WEKENI MTANDAO KATIKA MIJI MIDOGO – DC KIBONDO
TTCL WEKENI MTANDAO KATIKA MIJI MIDOGO – DC KIBONDO
By Prosper Kwigize | Published  10/6/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Kibondo
 
 Kampuni ya simu ya Tanzania TTCL imepewa changamoto kusambaza mawasiliano yake katika miji midogo wilayani Kibondo ili kuongeza kasi ya maendeleo na upashanaji habari.
 
 Wito huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Kibondo Luteni Kanal John Mzurikwao wakati akiongea na mkurugeni wa kampuni hiyo aliyetembelea ofisini kwake jana.
 
 Luteni kanali Mzurikwao ameeleza kuwa endapo miji ya Kakonko, Mabamba, Kasanda na Kifura itapelekewa mawasiliano ya simu ya TTCL wananchi na wafanyabiashara wataongeza kasi ya uchumi wao.
 
 Aidha ameuhamasisha uongozi wa kampuni hiyo kuboresha mahusiano na idara za serikali na kuongeza kuwa licha ya kampuni ya TTCL kuwa chini ya mwekezaji bado inabeba sura ya serikali.
 
 Akijibu sehemu ya maombi ya mkuu wa wilaya ya Kibondo mkurugenzi wa taifa wa TTCL Bw. Said Mkumba amesema kampuni yake tangu mwaka 2000 ilikwisha weak mkakati wa kitaifa wa kupanua mawasiliano yake hadi ngazi za miji midogo.
 
 Amebainisha kuwa kutokana na serikali kuingia ubia na makampuni mwengine ya uwekezaji ambapo serikli ilibaki na asilimia 65 ya uendeshaji mipango hiyo ya awali ilikwama kiutekelezaji.
 
 Aidha Bw. Mkumba amesisitiza kuwa kuanzia mwanzoni mwa mwaka huu tayari kampuni imerejea katika mipango yake ya awali ya kupanua mawasiliano na kuboresha mitambo yake katika wilaya zote nchini.
 
 Ameeleza kuwa kampuni inafanya zoezi la kuorodhesha miji midogo yote inayostahili kuwekewa mitambo ya simu za si waya ambazo ni rahisi kiuendeshaji na baadaye kupeleka wazo kwa bodi ya kampuni.
 
 Hata hivyo licha ya kuandaa utaratibu wa simu za si waya kwa miji midogo nchini, kampuni ya TTCL inatarajia kufungua huduma mpya ya simu itakayoambatana na mtandao wa internet wilayani Kibondo.
 
 Aidha wito umetolewa kwa watakao hitaji kuwa na mtandao wa simu za TTCL zenye mtandao wa internet kupeleka majina yao kwa afisa tawala wa wilaya au kwa meneja wa kampuni wa wilaya ili huduma hiyo itolewe haraka wilayani Kibondo.
 
 Kampuni ya simu Tanzania TTCL tayari inaendelea na ujenzi wa mitambo mipya katika wilaya za Kasulu na Kibondo ambapo pamoja na mambo mengine, kmpuni inatarajia kubadilisha mfumo mzima wa utendaji kazi.

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.