Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wakulima waua wafugaji watano Songwe, Chunya
Wakulima waua wafugaji watano Songwe, Chunya
By Habari Tanzania | Published  10/6/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Christopher Nyenyembe

MAPIGANO makali kati ya wakulima na wafugaji yaliyotokea Oktoba mosi, katika bonde la Songwe wilayani Chunya, yamesababisha mauaji ya watu watano.

Taarifa za uhakika zilizopatikana kutoka eneo la tukio na kutoka kwa viongozi wengine wa kiserikali na kijamii, zinaeleza kuwa waliouawa walikuwa ni sungusungu watano wa wafugaji na wengine kadhaa kujeruhiwa.

Hata hivyo taarifa zilizotolewa na Kamanda wa Polisi mkoani hapa, Suleiman Kova zinaeleza kuwa, waliouawa katika mapigano hayo ni sungusungu wawili na wengine 11walijeruhiwa vibaya.

Inadaiwa kuwa Sungusungu hao kutoka jamii ya wafugaji, walifikwa na mauti hayo kutokana na chuki ya muda mrefu iliyojengeka kutokana na tabia yao ya kulisha mifugo yao kwenye mashamba ya wakulima na wakulima kuiba mifugo yao kwa ajili ya kitoweo.

Kamanda Kova aliwataja sungusungu waliouawa kuwa ni Sinje Nkuba (20) na Sama Lula (15) na kuwa watu wanane wanashikiliwa kwa tuhuma za mauaji hayo na kujeruhi.

Kamanda Kova alisema sungusungu 200 wa jamii ya wafugaji kutoka Kijiji cha Nahaliongo, Kata ya Galula, walikivamia Kijiji cha Totowe kwa madai ya kusaka mifugo yao iliyoibwa.

Alisema sungusungu hao walipata taarifa kuwa, nyumba tatu katika kijiji hicho zilikuwa zimeficha nyama za ng’ombe wao baada ya kuwachinja.

Lova alisema baada ya kushindwa kuwakamata wenye nyumba hao, sungusungu hao walielekea eneo la vilabu vya pombe na kuanza kumpiga kila waliyemkuta kwenye eneo hilo.

Mapigano hayo yalisababisha wakulima saba kujeruhiwa na kupelekwa katika hospitali ya misheni ya Mwambani, walikopatiwa matibabu.

Kova alisema baada ya tukio hilo, sungusungu wengine wa Kijiji cha Manda wapatao 11 walipita kwenye Kijiji cha Totowe wakidai kuwa wameibiwa ng’ombe tisa.

Wananchi wa kijiji hicho walipogundua janja hiyo, wakulima hao waliamua kujihami kwa kuchukua mashoka, mapanga, virungu na fimbo na kuwashambulia sungusungu hao na kusababisha vifo hivyo.

Kamanda Kova aliwataja waliojeruhiwa na kulazwa kuwa ni Sophia Majengo (20), Cosmas Maiko (20), Kurwa Malae (20), Aluta Roda (34), Credo Wiliamu (36), Nicodem Paulo (42), Arcado Vungwa (28), Thadeo Jackson (54), Emmanuel Lwambo (40), Boni Cheupe (40) na Frolence Claudi (25).

Alisema hali kwenye eneo hilo imeendelea kuwa shwari baada ya kikosi cha kutuliza ghasia (FFU), kupelekwa kwenye eneo hilo kulinda usalama.

Mapigano kati ya wakulima na wafugaji yamekuwa ni jambo la kawaida katika maeneo mbalimbali hapa nchini.

Matukio hayo ambayo mara kadhaa yamekuwa yakisababisha madhara, yamekuwa yakitokea mkoani Morogoro, Arusha, Manyara na Mara.

Viongozi takriban wote wakuu tangu wa awamu ya tatu, wamekuwa wakijaribu mara kadhaa kuzungumzia hali hii, ikiwa ni pamoja na kuwaasa wakulima na wafugaji kuishi kwa kuvumiliana.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.