Habari Tanzania - http://www.habaritanzania.com
Tanzania vs Mozambique
http://www.habaritanzania.com/articles/1214/1/Tanzania-vs-Mozambique
By Marshy Abdu
Published on 10/6/2006
 
Timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars imeingia kambini kujiandaa na mechi yake ya pili dhidi ya kikosi cha Msumbiji. (Mozambique/Mocambique)

Tanzania vs Mozambique

Timu ya soka ya Taifa, Taifa Stars imeingia kambini kujiandaa na mechi yake ya pili dhidi ya kikosi cha Msumbiji.

Stars na Msumbiji wanatarajiwa kukutana kati ya Oktoba 6 na 8 huko Msumbiji katika mechi ya kundi la 12 ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Mataifa ya Afrika.

Fainali hizo zitakafanyika Ghana mwaka 2008 na Tanzania chini ya kocha mpya, Marcio Maximo inatarajia kufanya kila linalowezekana ili kufika huko.

Ifuatayo ni orodha ya majina kamili ya wachezaji waliochaguliwa kwa ajili ya kujiandaa na mchezo huo ambao utafanyika ugenini.

MAKIPA: Juma Kaseja (Simba), Ivo Mapunda (Yanga) na Japhary Said (KMKM ya Zanzibar).

MABEKI:Dickson Daudi (Mtibwa), Mecky Maxime (Mtibwa), Nadir Haruob (Yanga), Said Morad (Ashanti), Haji Mbelwa (Rayon), Salum Swedi (Mtibwa), Shadrack Nsajigwa (Yanga) na Victor Costa (Simba).


VIUNGO: Renatus Njohole (Baulmes), Athuman Idd (Simba), Henry Joseph (Simba), Hussein Sued (Ashanti), Marleges Mwangwa (Kagera Sugar), Nizar Khalfan (Mtibwa) na Obadia Mungusa (Mwenge).

WASHAMBULIAJI: Bakari Kigodeko (Ashanti), Gaudence Mwaikimba (Yanga), Mussa Mgosi (Simba), Said Maulid (Yanga) na Emmanuel Gabriel (Simba).

Pia Maximo aliwataja wachezaji vijana ambao ni Godfrey Sharuti, Yassin Juma, Mecky Michael na Jerry Tegete.

Katika mechi ya kwanza, Stars iliibamiza Burkinafaso mabao 2-1 na hivyo kuifanya Tanzania kupanda nafasi 28 katika orodha ya Shirikisho la  Soka  Afrika (CAF)na nafasi ya 105 Duniani (FIFA) 

Kila la Kheri Tanzania, Kila la Kheri Taifa Stars.

Habri Tanzania.com inasema kwamba watanzania shangilia ushindi unakuja