Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  CUF wafuatilia vikao vya siri vya Kikwete
CUF wafuatilia vikao vya siri vya Kikwete
By Habari Tanzania | Published  10/5/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Charles Mullinda

VIONGOZI wakuu wawili wa Chama cha Wananchi (CUF), Katibu Mkuu, Maalim Seif Sharif Hamad na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Hamad Rashid Mohammed wamesema, Rais Kikwete amekuwa akifanya juhudi kubwa za chini kwa chini katika kupata ufumbuzi wa mpasuko wa kisiasa wa Zanzibar.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti, juzi usiku na jana asubuhi, viongozi hao wawili wa CUF walieleza kupata taarifa kuhusu hatua hizo zisizo za wazi ambazo Rais Kikwete amekuwa akizichukua katika kupata ufumbuzi wa tatizo hilo.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu juzi usiku, Maalim Seif alisema taarifa alizonazo kuhusu hatua ambazo amekuwa akizichukua Kikwete kuhusu suala hilo la Zanzibar ni za kutia moyo.

“Bado hajakutana na sisi ingawa tumekuwa tukipata taarifa kila anapokutana na makundi mbalimbali ya watu na kwa kweli taarifa tulizonazo zinaonyesha amefikia mahali pazuri kama alivyosema yeye mwenyewe,” alisema Maalim Seif alipoulizwa iwapo alikuwa akijua lolote kuhusu hatua za Kikwete katika suala hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Hamad Rashid alisema wakati umefika kwa Rais Kikwete kueleza hadharani hatua aliyofikia katika kutafuta ufumbuzi wa mgogoro wa kisiasa Zanzibar.

Alisema kambi ya upinzani bungeni ina ushahidi kuwa Rais Kikwete amefanya jitihada za kutosha kutafuta ushauri kutoka kwa wasomi kadhaa wa chuo kikuu na watu wengine maarufu kuhusu namna ya kuutatua mgogoro huo.

“Wakati umefika kwa Rais Kikwete kuzishirikisha pande zinazosuguana kisiasa Zanzibar na kuweka bayana hatua aliyofikia kumaliza msuguano huo.

“Tunaamini na tuna ushahidi kuwa rais amefikia hatua nzuri, amekutana na baadhi ya wasomi wa chuo kikuu na watu wengine maarufu ambao amewaomba ushauri kuhusu kumaliza tatizo la kisiasa Zanzibar.

“Ni vizuri wahusika wakawa na taarifa za kinachoendelea kuliko ukimya uliopo, kwa sababu suala lenyewe ni muhimu na linawahusu Watanzania wote,” alisema Hamad.

Alisema CUF ina imani na Rais Kikwete kuwa anaweza kulimaliza tatizo hilo kutokana na jinsi alivyojipambanua tangu mwanzo wa uongozi wake kuwa ana uwezo huo.

“Kikwete ni rais wa kwanza baada ya Mwalimu Nyerere kuweza kuzungumzia kero kubwa ya Muungano waziwazi, huku makundi husika yakiwapo na baadhi ya viongozi walioshindwa kutatua tatizo hilo wakiwapo,” alisema Hamad.

Hata hivyo, alitahadharisha kwamba, Kikwete anapaswa kuwa wazi kama alivyokuwa katika hotuba aliyoitoa Desemba wakati akifumgua Bunge mjini Dodoma, ili kuondoa dhana inayotumiwa na wanasiasa kupotosha ukweli wa tatizo hilo.

Hamad alisema baadhi ya wanasiasa wanaudanganya ulimwengu kuwa tatizo la kisiasa Zanzibar linatokana na historia, jambo ambalo si kweli, bali linatumiwa na wanasiasa hao kwa manufaa yao ya kisiasa ili waendelee kutawala visiwa hivyo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.