Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Ikulu yashtuka Kikwete kukashfiwa tena Kenya
Ikulu yashtuka Kikwete kukashfiwa tena Kenya
By Habari Tanzania | Published  10/4/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
na Absalom Kibanda

OFISI ya Rais (Ikulu), imesema imeshtushwa na kushangazwa na katuni iliyochorwa katika gazeti la Kenya la Sunday Nation la Jumapili iliyopita inayomuonyesha Rais Jakaya Kikwete akilambwa viatu na waandishi wa vyombo vya habari hapa nchini.

Akizungumza na Tanzania Daima kwa simu jana, Mwandishi Msaidizi wa Habari wa Rais, Maura Mwingira alisema Ikulu imeiona picha hiyo na kuichukulia kuwa ni dhihaka mbaya kwa Rais Kikwete na kwa vyombo vya habari hapa nchini.

Mwingira alisema pamoja na kulitambua hilo, Rais Kikwete ameamua kukaa kimya akiendeleza msimamo wake wa kawaida wa kutotaka kuingia katika malumbano ya aina yoyote na vyombo vya habari.

“Ni kweli tumeiona ile katuni. Ni mbaya. Rais kama ilivyo kawaida yake hangependa kuendeleza malumbano na vyombo vya habari, lakini kwa kweli sasa hawa Wakenya wamefika pabaya kwani wameamua kumdhalilisha rais wetu aliyechaguliwa kwa asilimia 80 ya kura na Watanzania.

“Sisi Watanzania kwa hulka ni waungwana na watu tusiopenda malumbano kama ilivyo kwa wenzetu hao. Wanapaswa kutambua kuwa, Kikwete ni kiongozi wa nchi anayepaswa kuheshimiwa. Hata kama kuna uhuru wa vyombo vya habari, nadhani kwa katuni ile huo si uhuru, ni dharau,” alisema Maura.

Alisema pamoja na wao (Ikulu) kukaa kimya, ana imani kwamba, vyombo vya habari hapa nchini, vina wajibu wa kutokaa kimya katika hili kwani, katuni hiyo nayo inaonyesha kwamba waandishi wa habari wanamlamba Rais Kikwete viatu, jambo alilolielezea kuwa ni udhalilishaji wa taaluma ya uandishi.

Katuni hiyo imeendelea kuthibitisha kwa namna nyingine kwamba, kumekuwa na hali ya baadhi ya wananchi na viongozi wa Kenya kutoiamini na wakati mwingine kuonyesha dharau za wazi kwa Serikali ya Rais Kikwete.

Septemba 19 mwaka huu, vyombo vya habari vya Kenya vikiongozwa na gazeti la Nation ambalo ni gazeti dada la Sunday Nation, vililivalia njuga suala la mkutano kati ya Rais George W. Bush wa Marekani na Rais Kikwete uliofanyika New York, Marekani, muda mfupi kabla ya kuanza kwa kikao cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambacho Kikwete alihudhuria kwa mara ya kwanza akiwa rais.

Uamuzi wa Wakenya kuvalia njuga suala hilo ulikuja baada ya Mshauri wa Masuala ya Afrika wa Rais wa Marekani, Cindy Courville kuwaeleza waandishi wa habari kuwa, hali ya kukosekana kwa utangamano wa kisiasa nchini Kenya, lilikuwa moja ya mambo yaliyojadiliwa wakati wa mkutano wa viongozi hao wawili.

Taarifa hiyo ya Courville ilisababisha gazeti la Nation kuibua mjadala kuhusu suala hilo, hata kufika hatua ya kuandika maoni ya mhariri likihoji sababu za Bush kuijadili Kenya akiwa na Kikwete pasipo kuwashirikisha viongozi wa nchi hiyo (Kenya) waliokuwa wakiongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa nchi hiyo, Raphael Tuju aliyekuwapo huko huko New York.

Pamoja na taarifa za gazeti hilo kueleza katika sehemu fulani kwamba, Tanzania imekuwa na uhusiano mzuri na Kenya, hususan katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, maoni na habari zilizoandikwa katika gazeti hilo zilionyesha dhahiri dharau kwa Kikwete na Tanzania.

Mbali ya gazeti la Nation, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Kenya, Moses Wetang’ula naye aliingia na kueleza kushangazwa kwake na uamuzi huo wa Bush kuijadili Kenya akiwa na Kikwete na pia kuzungumzia hali ya kutotengemaa, wakati akijua kuwa nchi hiyo ilikuwa na amani na utulivu.

Akizungumza kuhusu suala hilo alipokuwa akizungumza na wahariri wakuu wa vyombo vya habari jijini Dar es Salaam juzi, Kikwete kwa ufupi na huku akisema ‘tusifike mbali zaidi’, alisema katika mazungumzo yao, Rais Bush alitaka tu kujua iwapo kelele za kisiasa anazosikia kutoka Kenya zitaendelea kuliacha taifa hilo katika hali ya amani.

“Nilichokiona mimi katika mazungumzo yale ni kwamba Rais Bush aliuliza kama rafiki na wala si zaidi ya hapo... tusifike mbali zaidi,” alisema Kikwete akionyesha namna ambavyo hakuwa tayari kueleza hisia zake waziwazi kuhusu suala hilo.

Kwa muda mrefu sasa na hasa tangu serikali ilipowafukuza waandishi wapatao sita wa habari wa Kenya, wote wakitokea gazeti la Nation, kwa kosa la kufanya kazi nchini kinyume cha sheria mapema mwaka jana, kumekuwa na uhusiano wa shaka kati ya nchi hizi mbili.

Miongoni mwa waandishi hao wa Kenya waliofukuzwa ni Mutuma Mathiu ambaye hivi sasa ndiye Mhariri Mtendaji wa gazeti la Sunday Nation ambalo juzi Jumapili limetumia katuni hiyo iliyobeba ujumbe wa dhihaka.

Wakati Nation wakiwatuhumu waandishi wa Tanzania kwa kuikumbatia Serikali ya Kikwete, gazeti hilo katika hali ya uwazi kabisa ndilo lililoongoza harakati za kuhakikisha Rais Mwai Kibaki na chama cha muungano wa vyama uliounda Narc wanaingia madarakani na kukibwaga chama cha Kanu ambacho ndicho kilichokuwa kikiongoza nchi hiyo tangu uhuru mwaka 1962.

Hata hivyo, tuhuma za rushwa na ukiukwaji wa misingi ya utawala bora vilisababisha magazeti hayo kulazimika kubadili msimamo wake wa kuiunga mkono Serikali ya Kibaki.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by sangiwa)
    Rating
    I think that Kenyans were not pleased with the fact that Tanzania has shown stability in its political growth.

    Tanzanian politics is not marred by violence to the extent that Kenya is. Not only that Kenya has enjoyed the spotlight for all these years in the international arena that being put in a place other than first is tough to swallow.

    Grow up Kenya,..!!!
     
  • Comment #2 (Posted by an unknown user)
    Rating
    i think our diplomats need to take care all of these before the state house do anything. what i think, both goverment has go good relation.If the state house jump to say anything, i thinks our diplomats fails.it is the sense of human always, if people discuss about you in ur absense, it will create some problem.
    So far our Media was to react before the state house.im sure most of our News Experts, they are not creative to look and fetch for infomation at earliest.u can image those two films, it came to be know this year, but the move was very long prepared and broadcasted in diffrent media.
     
  • Comment #3 (Posted by hamisa)
    Rating
    tatizo la kenya wameana kila wanalolifanya wananaswa kwenye mtego kama vile wizi wa mabenki magari. kikwete kasifiwa na wananchi wake kaongea na bush kwahiyo linawuma
     
  • Comment #4 (Posted by Proud Kenyan)
    Rating
    Tempted as I am to ask Tanzanian opinion to 'grow up', I will not. But pray me, why take cartoons that seriously? 15 years ago, cartoons like the one that is causing so much furore would have landed the cartoonist and his editor in police cells in Kenya. Today, no one bothers, and I guarantee that Kenya's president features in less than flattering cartoons at least once a week, in the mainstream newspapers!

    So, ndugu na dada WaTanzania, don't take such things too seriously if they come from Kenyans.

    And is the relationshup between Kenya and Tanzania really strained on account of the explusion of the six Kenyan journalists from the Nation Media Group? I don't think so. In my opinion, the strain, real or imagined, goes back way back, to the 1970s at least.

    Finally, Kenya became independent in 1963, not 1962.
     
  • Comment #5 (Posted by Kibeso Mwakinepule)
    Rating
    That thug GADO should not be allowed to come back to Tz, should stay there with his masters.He is uncoolthy, uncultured,and i will celebrate to hear that he has gone to hell!!!That son of a bitch!!!!!!Mwanaizaya
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.