Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Rais apewa shahada ya heshima, sasa ni Dk Kikwete
Rais apewa shahada ya heshima, sasa ni Dk Kikwete
By Habari Tanzania | Published  09/30/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:

Na Maura Mwingira, Minnesota, Marekani
Chuo Kikuu cha Mtakatifu Thomas, cha Minneapolis, Minnesota, kimemtunukia, Rais Jakaya Kikwete shahada ya heshima udaktari wa Falsafa (PhD) katika fani ya sheria.

Rais Jakaya Kikwete alitunukiwa shahada hiyo katika hafla iliyofanyika katika Chuo Kikuu hicho Alhamisi na na kushuhudiwa na mkewe, Mama Salma Kikwete, Ujumbe wa Rais uliokuwa umefuatana naye katika ziara hiyo, viongozi wakuu cha chuo hicho, wanafunzi na baadhi ya Watanzania wanaoishi katika mji wa Minneapolis, ulioko katika Jimbo la Minnesota.

Akitangaza uamuzi wa chuo hicho kumtunukia rais shahada hiyo, Mkuu wa Chuo Kikuu hicho, kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki, Father Dennis Dease, alisema kuwa Bodi ya uongozi wa Chuo hicho, uliamua kumtunuku shahada hiyo uongozi wa kutukuka na wa muda mrefu Serikalini, mwelekeo mzuri alioonyesha katika kuipeleka mbele Tanzania, ari aliyoonyesha katika kuwatumikia Watanzania tangu alipoingia madarakani, na ushindi mkubwa wa asilimia 80 alioupata wakati wa Uchaguzi Mkuu.

"Tunaamini siku moja si tu utakuwa na uwezo wa kutembea bali kukimbia, na watu wako watapata maendeleo yanayoendana na ile kauli mbiu yenu, uhuru na umoja na leo hii tunapokutunuku shahada hii ya heshima, tunasema Mungu Ibariki Tanzania," alisema Dease.

Mkuu huyo wa chuo alitoa changamoto kwa wanafunzi wengi wa Kitanzania kwenda kusoma katika chuo hicho, akibainisha kwamba wengi wa wanafunzi wanaosoma hapo wanatoka Kenya na Uganda.

Akizungumza mara baada ya kutunukiwa shahada hiyo, Rais Kikwete alisema ingawa ameingia madarakani muda mfupi tu uliopita kustahili kutunukiwa degree hiyo, lakini najua uamuzi huo umetokana na uongozi wa chuo kuwathamini Watanzania.

Alibainisha kutunukiwa kwake shahada hiyo ni kichocheo kwake yeye na Watanzania, wake kwa waume, kuendeleza misingi mizuri inayoshabihiana na ile ya chuo hicho.

Kabla ya kutunukiwa shahada hiyo, Rais Kikwete alikutana na baadhi ya wakurungezi wakuu wa makampuni ya biashara ya kimataifa, yenye makao yake Minnesota,.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.