Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wafanyabiashara wakubwa Dar huwatumia wachuuzi kukwepa kodi
Wafanyabiashara wakubwa Dar huwatumia wachuuzi kukwepa kodi
By Habari Tanzania | Published  09/30/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Stella Nyemenohi

Wachuuzi wadogowadogo wa biashara maarufu kwa jina la 'wamachinga' waliozagaa katika jiji la Dar es Salaam wanatumiwa na wafanyabiashara wakubwa na watumishi wa serikali.

Taarifa hiyo imetolewa jana zikiwa zimebaki saa chache wamachinga hao kuonekana katikakati ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kipindi cha miezi sita kilichotolewa na serikali kwa wachuuzi hao kuhama katika maeneo yasiyoruhusiwa kuendesha biashara hiyo.

Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, John Lubuva serikali, alisema jana kuwa asasi mbalimbali na wafanyabiashara wakubwa ndio wamiliki wakubwa wa bidhaa zinazouzwa mitaani huku wakitumia mgongo wa wamachinga.

Kutokana na hali hiyo, Halmashauri ya Manispaa ya Ilala imesema inafanya uchambuzi wa kina utakaowezesha kuchuja watu wasiostahili kupewa bure maeneo ya biashara kama inavyofanyika kwa wamachinga.

Aliyasema hayo juzi wakati akitoa taarifa kwenye mkutano wa dharura wa Baraza la Madiwani ambao ajenda yake kubwa ilikuwa juu ya operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara hao inayoanza leo.

Akizungumzia matatizo yanayoikabili halmashauri yake, Lubuva alisema manispaa imebaini kuwepo udanganyifu wa baadhi ya watumishi na wafanyabiashara wakubwa kumiliki biashara zilizoko mtaani huku zikidhaniwa ni za wafanyabiashara ndogondogo.

Lubuva alionyesha wasiwasi kuwa kuna uwezekano wa maeneo ya biashara yanayoandaliwa na manispaa, yakatumiwa na kundi hilo kuhamishia bidhaa zao zinazostahili kulipiwa ushuru katika maduka makubwa.

"Tunafanya uchambuzi ili isije ikawa maeneo tuliyotenga yakatumiwa na watu wenye uwezo kwa sababu wengine wana uwezo wa kukodisha majengo," alisema Lubuva.

Mbali na kauli hiyo ya Lubuva, baadhi ya wafanyabiashara katika soko la Mchikichini walilalamikia kile walichodai kuwa wenye maduka makubwa katika mitaa ya Kongo na Msimbazi, wamekuwa wakiwatumia wamachinga kuuza bidhaa zao mitaani.

Wakati huo huo, Andrew Msechu anaripoti kuwa
maeneo mengi waliyotengewa wamachinga yamevamiwa na wasio walengwa na kuwafanya walengwa katika zoezi hilo kutopata nafasi.

Hayo yalibainika jana wakati wa ziara ya Mwenyekiti wa Tanzania Labour Party (TLP), Augustine Lyatonga Mrema, katika maeneo ya Kigogo Sambusa na Tazara yaliyotengwa kwa ajili ya wafanyabiashara hao.

Mrema alisema serikali ina kila sababu kuongeza muda huo kwa kuwa agizo hilo limekuwa gumu kutekelezeka kwa watendaji wa Serikali.

"Hatupingi agizo la serikali, tunatambua kuwa ni lazima miji iwekwe kwenye mazingira yenye utaratibu unaoeleweka, lakini inashangaza kufikia leo katika maeneo yote hakuna kilichokamilika, hivi tunavyoongea vyoo ndiyo kwanza vinajengwa, hawa watu wataishi vipi katika maeneo haya?" alihoji.

Aliongeza kuwa Manispaa zilitakiwa kuhakikisha kuwa zinakamilisha ujenzi wa miundombinu katika maeneo hayo ikiwemo ujenzi wa vituo vya Polisi, stoo, njia za kupita, vyoo, umeme na maji ndipo wahimize uhamiaji wa wafanyabiashara hao.

"Ni suala la kushangaza, hili eneo la Kogogo Sambusa hakuna hata ramani, kinajengwa choo ambacho leo ndiyo kinapauliwa kukiwa hakuna maji, nina mashaka kuwa Waziri Mkuu anadanganywa na watendaji wake ambao tayari wanaonekana kushindwa kutekeleza agizo lake," alisema Mrema.

Mwenyekiti wa Kamati ya wafanyabiashara ndogo ndogo wa Kariakoo, Omaro Bakari, alisema yeye na wenzake wako tayari kuhamia katika maeneo hayo lakini akaomba kuwekewa huduma muhimu.

Moja wa wafanyabiashara hao katika eneo hilo jipya la Tazara Bashiru Mkuchika alisema idadi kubwa ya wafanyabiashara wa Tazara haijapata maeneo katika eneo hilo jipya na kuitaka serikali kuwatafutia maeneo mengine.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.