Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  JK anachangamkia fedha nje - Lowassa
JK anachangamkia fedha nje - Lowassa
By Habari Tanzania | Published  09/28/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na James Marenga, Iringa

WAZIRI Mkuu, Edward Lowassa kwa mara nyingine ametetea safari za Rais Jakaya Kikwete nje ya nchi na kusema anachofanya huko na hasa Marekani ni kuchangamkia fedha za Millennium Challenge Account takribani sh bilioni moja.

“Hata kama kuna watu wanaichukia Marekani, lakini ukweli unabaki pale pale kuwa Marekani ni taifa kubwa na Rais Bush tayari amekwishaonyesha nia ya kufanya kazi na Tanzania kwenye shughuli mbalimbali za maendeleo,” alisema Lowassa.

Alisema kama watu walikuwa wakifuatilia kwenye vyombo vya habari, hivi karibuni Rais Bush alimwambia Rais Kikwete kuwa yeye ni rafiki yake Afrika, na ameahidi kufanya naye kazi.

“Hawa mabwana wana fedha nyingi na sisi shida yetu ni kupata fedha nyingi kutimiza ahadi yetu kwa wananchi tuliyoitoa wakati wa kampeni za Uchaguzi Mkuu, hivyo wanaosema rais anakwenda huko kupoteza muda wanakosea, anatafuta fedha," alisitiza Lowassa.

Tanzania tayari imekwishapita kwenye hatua ya kwanza ya kupata fedha kwenye mfuko huo wa Marekani na hatua ya kwanza iliyofanywa na Marekani ni kutoa fedha kwa ajili ya kupambana na rushwa.

“Halafu mtambue kuwa huko aliko rais ndiko vipo hivi vyombo vikubwa vya fedha kama Benki ya Dunia na IMF na Tanzania tayari imeonekana kuwa inaweza kufanya vizuri kwenye mabadiliko ya uchumi, lazima tuchangamke,” alisema.

Akijibu baadhi ya kero za wananchi wa manispaa, aliagiza Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Vyuo Vikuu kuhakikisha inawapa wanafunzi walioidhinishwa kupewa mikopo hiyo mara moja.

Aliwataka pia viongozi wa halmashauri hasa wanaoshughulikia suala la ardhi kumaliza migogoro iliyojikita kwenye manispaa hiyo inayohusu ardhi.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Kamaliza Jumanne)
    Rating
    Ama kweli alisema Marehemu Mwalimu Nyerere kuwa mtu akikwambia suala la kipumbavu nawe ukakubali basi anakufanya wewe mpumbavu. Lowassa anamdanganya nani hapa? Hajui kuwa tunajua kuwa safari ndefu kama anayoendelea kuifanya Jakaya inaweza kugharimu hata zaidi ya hiyo bilioni moja?
    unatumia bilioni moja kwenda kuchangisha bilioni moja! Huu siyo wizi ndani ya wizi!
    Lowassa aambiwe aache ushamba asidhani wote ni mambumbumbu kama wapiga kura wake.
    Kwanza angetueleza nini maoni yake kuhusu tuhuma alizoachiwa na Mwalimu kuwa amejilimbikizia mali nyingi ya wizi.
    JK
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.