Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Maaskofu wapewa siku tano kujisalimisha
Maaskofu wapewa siku tano kujisalimisha
By Habari Tanzania | Published  09/28/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Kenneth Mwazembe, Mbozi

UMOJA wa Makanisa ya Kikristo wilayani hapa, mkoani Mbeya, umetoa siku saba kwa wachungaji na maaskofu wanaojihusisha na vitendo vya ujambazi na dawa za kulevya kujisalimisha polisi kabla hawajaanza kutajwa.

Kauli hiyo imetolewa juzi na washiriki wa semina ya siku tatu iliyoandaliwa na umoja huo, waliosema kuwa wapo miongoni mwa wachungaji wanaojihusisha na vitendo viovu ukiwamo ujambazi wa kutumia silaha, uuzaji wa dawa za kulevya na kueneza virusi vya UKIMWI.

Wakinukuu aya ya Biblia, wamesema ni vema waanze kutoa vibanzi kwenye macho yao ndipo wataweza kutoa kwa wengine, hivyo wametoa siku saba za kujisalimisha, baada ya hapo wataanza kuwataja watuhumiwa kwa kupeleka taarifa zao kwa Mkuu wa Wilaya.

Akizungumza wakati wa ufungaji wa semina hiyo, Mwenyekiti wa umoja huo, Mchungaji Burton Msongole, alisema maazimio hayo yamefikiwa kutokana na kukithiri kwa vitendo hivyo ambavyo vinaiathiri jamii.

Alisema kuwa wameamua kuchukua hatua hiyo baada ya kukerwa na tabia ya baadhi ya wenzao ambao wanafahamika, ambao wanaitia doa kazi ya Mungu


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.