Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Familia zilizotupiwa virago zarudi ndani
Familia zilizotupiwa virago zarudi ndani
By Habari Tanzania | Published  05/25/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mbazigwa Hassan

HATIMAYE familia nane za wapangaji zilizotupwa nje kwa nguvu katika nyumba namba 30 mtaa wa Nzasa, Ilala,Dar es Salaam zimerudishwa ndani jana kwa amri ya Mahakama ya Ardhi na Nyumba.

Familia hizo zimesota kuanzia Jumatano iliyopita kwa kulala nje kwa wiki moja kwenye baraza za nyumba jirani hadi jana walipoingia katika nyumba hiyo.

Kurudishwa kwa wapangaji hao kumefanywa na dalali wa Mahakama hiyo ya wilaya ya Ilala jana saa 5 asubuhi baada ya utekelezaji huo kushindikana Jumatatu na Jumanne wiki hii baada ya askari wa kampuni binafsi ya ulinzi kukataa kupokea hati ya mahakama hiyo.

Wakizungumza na mwandishi wa habari hii jana wakiwa ndani ya nyumba hiyo wapangaji hao akiwemo Khalfani Baweni ambaye ni mmiliki wa nyumba hiyo ya urithi walisema kuwa dalali wa mahakama alivunja mlango na kuwaruhusu kuingia pamoja na mali zao.

Walisema askari wa kampuni binafsi ya Mbelwa 05, walipoona kitendo hicho walikwenda polisi kuomba msaada lakini waligonga mwamba na waliporejea waliikuta kazi hiyo ikiendelea katika hali ya utulivu.Hadi jana saa 8 mchana askari hao walikuwa katika eneo hilo.

Wakizungumzia hasara waliyoipata, Baweni alidai baada ya kuingia chumbani aligundua kuwa amepoteza sh.milioni 2.3,Monono Swai sh.milioni tatu,wakati Mwashamba Shabani alidai kapoteza sh.milioni 1.7 pamoja na vito vya dhahabu vyenye thamani ya sh.100,000.

Pia walidai kuwa vifaa kadhaa vikiwemo vyombo vya nyumbani ambavyo hawakutaja thamani yake kuwa vimepotea na kuongeza kuwa milango ya vyumba vitatu ya nyumba hiyo ilivunjwa na kuwekwa sebuleni.

Walidai kuwa mvua iliyonyesha usiku wa kuamkia jana ilichangia katika kuharibu baadhi ya vifaa na kuongeza kuwa kazi ya kupanga vifaa ilikuwa inafanyika upya baada ya kutawanyika ndani na uwani mwa nyumba hiyo.

Mwandishi wa habari hii aliyefika hapo jana mchana aliwakuta wapangaji Saidi Pembe na Swai wakifanya matengenezo katika choo na kurudishia bati kwenye paa uharibifu waliodai ulifanyika siku waliyoondolewa.

Hati ya Mahakama ya Ardhi na Nyumba ya Mei22,mwaka huu iliyotoa amri ya kuwarudisha wapangaji hao ambayo nakala yake alipewa mnunuzi wa nyumba hiyo Yasin Mohamed Mussa na mmiliki Baweni,inaonyesha kuwa shauri hilo litasikilizwa Juni 6,2006.

Familia hizo nane ziliondolewa na kundi la vijana 40 waliodaiwa kuifanya kazi hiyo kwa kibali cha Mahakama ya Mwanzo bila wapangaji kupewa notisi kwa madai ya kuuzwa kwa Mpemba.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.