Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Mitandao kumi ya Mapanki yafungwa
Mitandao kumi ya Mapanki yafungwa
By Seif Mangwangi | Published  09/28/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Na Mwandishi wa HabariTanzania.com
Mitandao hiyo iliyotengenezwa maalum kwaajili ya kupingana na filamu ya Darwins night mare inayoonyesha namna ambavyo wakazi wa jiji la Mwanza wanavyokula masalia ya samaki maarufu kama Mapanki imefungwa kuanzia jana.
 
 Mitandao hiyo inaonyesha kushindwa kujiendesha baada ya kukosa fedha na imeandikwa maneno ya (This account has been suspended,Please contact the billing/support department as soon as possible).
 
 Kufuatia kufungwa kwa mitandao hiyo watu mbalimbali waliokuwa wakiitembelea kote duniani watashindwa kujua ukweli kuhusu filamu ya mapanki ambayo imekuwa ikipoteza soko la samaki la Tanzania nje ya nchi.
 
 Filamu ya Darwinsnightmare iliyotengenezwa na mwandishi wa habari wa kujitegemea Bw.Hurber Souper raia wa nchi ya Austria anayeishi nchini Ufaransa imekuwa ikieleza mabaya kuhusiana na soko la Samaki aina ya Sangara ambapo alidai kwamba watanzania wamekuwa wakila mabaki ya samaki maarufu kama ‘mapanki’ huku minofu ya samaki hao ikisafirishwa kwenda bara ulaya na Asia.
 
 Pia ndani ya filamu hiyo yenye dakika 107 imeeleza hali ya umasikini uliokithiri nchini Tanzania, umalaya unaofanywa na watanzania kutokana na uduni wa maisha waliokuwa nao, watoto wa mitaani na biashara ya silaha katika nchi za maziwa makuu ikiwemo Tanzania.
 
 Ndani ya mitandao hiyo kumi iliyotengenezwa na watanzania wenye nia nzuri na nchi yao kulikuwa na tamko la Serikali la kupingana na filamu ya mapanki na nyaraka mbalimbali za Serikali na za kimataifa ambazo zote zilikuwa zikielezea hali halisi ya shughuli za uvuvi katika ziwa Victoria na vivutio vya utalii na uwekezaji nchini Tanzania.
 
 Mitandao hiyo iliweza kuingilia mtandao wa Bw.Hubert Souper unaoonyesha filamu hiyo na kuweza kushusha soko la filamu hiyo baada ya watu wengi kutembelea mitandao ya watanzania hao na kujua ukweli kuhusiana na suala la samaki wanaovuliwa katika ziwa Victoria.
 
 Kwa mujibu wa mtandao Mama kati ya mitandao kumi iliyotengenezwa na watanzania hao wa www.darwinsnightmare.net umekuwa ukionyesha kuwa mitandao hiyo imekuwa ikitembelewa na zaidi ya watu milioni mbili kwa siku kote duniani.
 
 Matangazo ya mitandao hiyo pia yamekuwa yakionekana katika mitandao mikubwa duniani (search engine), kama vile mitandao ya Yahoo, Google, MSN, Info seek, na mitandao rafiki (Partner web sites), zaidi ya milioni 19 duniani.
 
 Mitandao mingine iliyotengenezwa na watanzania hao na ambayo ilikuwa ikipatikana kote duniani ni pamoja na www.darwinsnightmare.us, www.darwinsnightmare.ws
 www.darwinsnightmare.co.uk,www.darwinsnightmare.eu,www.darwinsnightmare.info,
 www.darwinsnightmare.co.tz , www.darwinsnightmare.org, www.darwinsnighmare.biz, www.darwinsnightmare.name.
 
 Kupitia katika mitandao hiyo watu mbalimbali walikuwa wakitoa maoni yao hususani wafanyabiashara wa samaki katika bara la ulaya na walaji wa samaki nchini ambao wamekuwa wakilaani vikali filamu ya mapanki.
 
 Watu mbalimbali waliozungumza na majira kuhusu kufungwa kwa mitandao hiyo jana mjini hapa waliiomba Serikali na sekta binafsi kuingilia kati kufungwa kwa mitandao hiyo ili kuokoa soko la samaki na kuiletea heshima nchi ya Tanzania.
 
 Baada ya Bw.Hubert Souper kutegenezaa filamu ya Darwinsnightmare Rais Jakaya Kikwete, Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wananchi mbalimbali wakiwemo wa Mkoa wa Mwanza walilaani vikali filamu hiyo na kutangaza mikakati mbalimbali ya kuipinga.
 
 Watanzania waliotengeneza mitandao hiyo ya kupinga filamu ya Bw.Huber Souper walipotafutwa kuzungumzia kufungwa kwa mitandao hiyo na gharama ambayo inahitaji walishindwa kupatikana baada ya simu zao zote kufungwa.
 

How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments
  • Comment #1 (Posted by Anon)
    Rating
    !?!
     
  • Comment #2 (Posted by Prosper Kwigize)
    Rating
    Haina maana yoyote kwa Tanzania kukaa kimya wakati watetezi wa utaifa wenye uzalendo wakikwama kwa sababu tu wamekosa pesa, Hata mimi nimeumia sana kuona mtandao huo wa wapinga Mapanki (wanaompinga Hubert) wakifungiwa mitandao yao ambayo kimsingi ni ya watanzania wote. Serikali inapaswa kuingilia kati kulipia mitandao hiyo ili kurejesha heshima ya tanzania iliyodharirishwa duniani kote.
     
  • Comment #3 (Posted by Bernard Rabiel)
    Rating
    Ni kwa masikitiko makubwa kuona wenzetu wameshindwa kuendesha mitandao hiyo. jambo la kushukuru ni kuwa wameonyesha jitihada ya kuipigania nchi yao.
    Hivyo nadhani tuangalie njia ya kuwasaidia.
     
  • Comment #4 (Posted by hassan)
    Rating
    good story
     
Submit Comment


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.