Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Wasomali waibuliwa kutoka mafichoni
Wasomali waibuliwa kutoka mafichoni
By Habari Tanzania | Published  09/27/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
Na Mussa Juma, Arusha
Raia saba wa Somalia wanaotuhumiwa kuingia Tanzania kinyemela wamekamatwa baada ya maofisi wa Uhamijai kuvunja chumba walimokuwa wamefichwa mjini Arusha, Kaskazini ya Tanzania.

Afisa Uhamiaji wa Mkoa wa Arusha, Justin Kabugumila jana alisema Wasomali hao waliokamatwa, wawili ni watu wazima na watoto wanaodai kuwa ni yatima baada ya wazazi wao kuuawa katika vita vinavyoendelea nchini kwao.

Wasomali hao wanadaiwa kukamatwa Jumapili iliyopita majira ya alasiri baada ya maafisa hao wa idara hiyo kwa kushirikiana na askari wa jeshi la polisi mkoani hapa.

Baada ya kuwahoji watoto hao walidai kuwa waliingia nchini kwa lengo la kwenda kumtafuta baba yao mdogo aishiye jijini Dar es Salaam baada ya kufiwa na wazazi wao.Kukamatwa kwa raia hao, kunafuatia taarifa kutoka kwa raia mwema baada ya kuwaona wakiingizwa kwenye chumba hicho na kufungiwa kwa nje.

Inadaiwa waliingizwa nchini na watoto wa mwenye nyumba hiyo.Watuhumiwa wawili ambao wenye umri juu zaidi ya miaka 18 watafikishwa mahakamani kujibu mashtaka ya kuingia nchini kinyemela huku polisi ikiendelea kuwasaka watoto wa mwenye nyumba hiyo kwa tuhuma za kuwaingiza nchini Wasomali hao kinyume cha sheria.

"Hawa wengine (watoto) bado tunafanya mahojiano nao kujua ndugu zao kama kweli mmoja yupo Dar es Salaam au kama wana ndugu Nairobi Kenya ili tuwarejeshe, "alisema.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
This article has been added to your 'Articles to Read' list.
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.