Na Epson Luhwago
BODI ya Usajili wa Wahandisi nchini (ERB) kwa kushirikiana na Chama cha Wahandisi Washauri Tanzania (ACET), imeandaa mkutano wa siku moja kujadili pamoja na mambo mengine kuporomoka kwa jengo la ghorofa tano la Chang'ombe, Dar es Salaam.
Kaimu Msajili wa ERB, Injinia Steven Mlote, aliwaambia waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam kuwa k atika mkutano huo utakaofanyika kwenye hoteli ya Kunduchi Beach and Resort, Dar es Salaam pia Bodi itatoa taarifa ya juu ya mambo iliyoyaona wakati wa
ukaguzi wa majengo mbalimbali nchini.
"Bodi kwa kushirikiana na ACET tumeona ni vyemakuandaa mkutano huu ili kukumbushana mambo mbalimbalikutokana na hali ilivyo sasa katika shughuli zakihandisi na matukio ya hivi karibuni," alisema.
Injinia Mlote alisema hatua hiyo pia imechukuliwa ilikuwakumbusha wahandisi na wadau wa ujenzi juu yataaluma na kazi za kihandisi kwa maendeleo ya taifa.
Alisema katika mkutano huo utakaohusisha wahandisiwashauri, madhumuni hasa ya mkutano huo wa mashauriano ni kuweka mtandao baina ya wahandisi washauri ilikuwasaidia kubadilishana ujuzi na uzoefu katika kazi zao.
Kaimu Msajili alisema nia hasa juu ya hilo nikuimarisha kazi ya ushauri wa kihandisi na usimamiziwa ujenzi katika shughuli za ujenzi kwenye maeneombalimbali nchini.
"Lengo la mkutano huu pia ni kuwakumbusha wahandisiwashauri juu ya vigezo vinavyotakiwa katika shughulizao kwa mujibu wa Sheria ya Usajili wa Wahandisi, taratibu, miiko na maadili ya wahandisi," aliongeza.
Mlote alisema hivi karibuni kumejitokeza matukioyasiyofuata taratibu, sheria na maadili ya taaluma yauhandisi miongoni mwa wahandisi na wahandisi washauri,hivyo kusababisha hadhira mbaya kwa jamii juu yamwenendo mzima wa taaluma ya kihandisi.
Katika mkutano huo, kwa mujibu wa Mlote, wahandisiwashauri wataelezwa taarifa juu ya vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya kazi vinavyofanywa na baadhi ya wahandisi washauri.
Injinia Mlote alisema mkutano huo wa aina yake katikataaluma na fani ya uhandisi, pia utahudhuriwa na wahandisi wataalam wa muda mrefu hapa nchini.