Chuo kikuu cha Mtakatifu Agostino SAUT cha jijini Mwnza kimetangaza rasimi kuungana na serikali kipinga kikamilifu filamu ya Darwin's NightMare maarufu kama filamu ya mapanki.
Makamu mkuu wa chuo hicho Padre Dr. Charles Kitima ametangtaza msimamo huo mwishoni mwa wiki wakati wa mahafali ya tisa ya kozi ya uandishi wa habari za mazingira na mawsiliano yanayofanyika chuoni hapo.
Dr. Kitima amesema chuo kinasikitishwa sana na kitendo cha mwandishi wa filamu hiyo Bw. Hebert Sauper cha kulizalilisha ziwa Victoria ambalo hutegemewa na watanzania wengi kuwalishe na pato.
Aidha ametoa wito kwa wanahabari wa Tanzania kuungana pamoja kulitangaza ziwa Victoria ili liendelee kuwa kivutio kwa wananchi na watalii pamoja na wafanyabiashara wa samaki wa ndani na nje.
Ameongeza kuwa chuo cha SAUT kwa muda mrefu kimekuwa kikitoa mafunzo ya habari za mazingira sambamba na kulitangaza ziwa Victoria pamoja na kufanya tafiti mbalimbali ambazo zimeleta mafanikio.
Padre Kitima amefahamisha kuwa mwaka 2003 kabla ya sakata la filamu ya mapanki chuo hicho tayali kilikwisha fanya tafiti kadhaa kuyahusu mapanki na kushuhudia jinsi wananchi wanavyoyaandaa kabla ya kuyauza.
Hata hivyo ametoa wito kwa serikali kuwa makini wanaporuhusu wageni kuingia ndani ya nchi yetu ili kuepusha uwezekano wa wageni kufanya kazi zisizo na maslahi kwa watanzania kama ilivyotokea kwa Hubert Sauper.
Comments
Comment #1
(Posted by nthelezi nesaa) Rating
Japo ni uhuru wa ntu kutoa mawazo yake, kuna haja ya wakuu wa taasisi kutofautisha maoni binafsi na ya taasisi zao,
Mazingira yanaonyesha mkuu wa chuo alitoa mawazo yake. Hili ni sawa kwa upande wa chuo tulitegemea wanafunzi kupitia uongozi wao watoe tamko.
Kuitangaza Mwanza ni bora kama matokeo ya ufanisi hayataishia kwenye matumbo ya manyang'au wetu.
Leo tunaikimbia Nightmare kesho inazaliwa Slavery!
Yote hii ni kwa sababu ya kuwa na serikali zisizo na mipango madhubuti kwa ajili ya watu wake.
Jamani tuzidi kushinikiza kieleweke.
Comment #2
(Posted by eva) Rating
mimi siwaelewi wewe unapesa yako sh.100kwanini unakubali kununua kitu ambacho huwezi kula kimeoza hayo ni yakweli kuwa wasukuma wanakula samaki aliyeoza wakati kuna mbonga zingine hebu tufikilie jamani nani anaweza kutoa fedha yake kununua kitu kibovu.mimi hiyo film nimeiona naona ni kutunga kwa vile njeyetu ni masikini ndio maana tumeona kuwa wametudhailisha