Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Lowassa achangia mamilioni Dar
Lowassa achangia mamilioni Dar
By Habari Tanzania | Published  09/25/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Dina Zubeiry

WAZIRI Mkuu, Edward Ngoyai Lowassa, juzi aliwateka wadau wa michezo, hususani soka waliojitokeza kuchangia ujenzi wa shule ya sekondari ya michezo iliyopo Kigamboni, Dar es Salaam baada ya kuchangia sh mil. 60 kati ya sh 88,340,000 zilizopatikana.

Hata hivyo, Lowassa aliyetarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski hakuwapo kutokana na majukumu ya kitaifa kwani alikuwa Arusha kwa shughuli za kiserikali hivyo kuwakilishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Joel Bendera.

Akizungumza kwa niaba ya wadhamni wa ujenzi huo, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA), Mufti wa Tanzania, Shaaban bin Issa Simba, alisema kwamba Lowassa ameahidi kuchanga kiasi hicho cha fedha, pia ataandaa hafla nyingine ya kuchangia shule hiyo baada ya kumalizika kwa mfungo wa Ramadhani.

Aidha, Mufti alisema wameahirisha pia kazi ya utoaji tuzo kwa wadau mbalimbali waliotoa mchango katika sekta ya michezo pamoja na mnada wa picha na nguo za michezo za Rais Jakaya Kikwete mpaka kwenye hafla hiyo ya Lowassa.

Mbali ya Waziri Mkuu, wadau wengine waliojitokeza kuchangia ni pamoja na wakazi wa Kijiji cha Soga, Kibaha waliotoa shamba la hekari 100 kwa kuliuza kwa gharama ya sh mil. 15, Kampuni ya Cargo Stars imetoa sh mil. 2 na mifuko 200 ya saruji.

Wengine waliochangia ni Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), sh mil. 5, wadau wengine wawili ambao hawakupenda kutajwa majina yao walichangia sh mil. 5 kila mmoja, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe na familia yake alichanga sh mil. 2 wakati kwa upande wa chama walichanga sh milioni moja.

Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) lilichangia sh milioni 2, wakati Bendera, Benki ya Akiba Commercial (ACB), Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) walichanga sh. mil 1 kila mmoja, Luteni Jenerali Davis Mwamunyange na Mkurugenzi wa CxC Holdings, Charles Hamka walichanga sh 500,000 kila mmoja.

Wengine waliochangia sh 100,000 kila mmoja ni Mfuko wa Mwalimu Nyerere (MNF), Meneja Uhusiano wa Benki ya Taifa ya Makabwela (NMB), Shy-Rose Bhanji pamoja na mke wa Mwenyekiti wa Taasisi ya Tanzania Sports Catalyst (TASCA), inayosimamia ujenzi huo, Suleiman Mathew wakati Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Iddi Kipingu alichanga sh 20,000 huku watoto Anitha Mathew na Gatano Mathew kila mmoja alichanga sh 10,000.

Mathew aliwashukuru wote waliojitokeza kuchangia na kuomba waendelee na moyo huo kwani utasaidia maendeleo ya michezo na kusema kuwa fedha hizo zitatumika kwa madhumuni yaliyokusudiwa na si vinginevyo.

Baadhi ya wadau waliohudhuria hafla hiyo ni pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group, Yussuf Manji, Mkurugenzi wa ITV, Joyce Mhaville, Kamishna Msaidizi wa Polisi Kanda ya Dar es Salaam, Abdallah Msika, Mkurugenzi wa African Stars Entertainment (ASET), Asha Baraka, Mkurugenzi wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Sunday Kayuni na wengine


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.