Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Matatizo yazidi kukiandama Chuo Kikuu Dar
Matatizo yazidi kukiandama Chuo Kikuu Dar
By Habari Tanzania | Published  09/25/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Stella Nyemenohi
WAKATI wimbi la mgogoro wa mikopo ya wanafunzi likiendelea kukitikisa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), wanataaluma wa chuo hicho nao wameibuka wakikitaka chuo hicho kuboresha mazingira ili kunusuru mustakhabali wa elimu chuoni hapo.Kundi hili linalohusisha wahadhiri wasaidizi, limeamua kuvunja ukimya kwa kuweka wazi kero na matatizo yanayowakabili, huku suala la kuwezeshwa kupata digrii ya Udaktari wa Falsafa (PhD) likiwa miongoni mwa mambo yaliyowekwa mbele.

Wiki iliyopita, wanataaluma hao chini ya viongozi wao, Kitila Mkumba na Bashiru Ally, walifanya mkutano uliodumu kwa zaidi ya saa nne, uliofuatiwa na kuundwa kwa kamati ya watu 20 ya kufuatilia kero mbalimbali wanazotaka zitatuliwe na uongozi wa chuo.DSM kimewagawa wafanyakazi wake katika makundi matano ambao ni wahadhiri wasaidizi, wahadhiri, wahadhiri waandamizi, maprofesa washiriki na maprofesa kamili.

Katika madai yao, wanataaluma hao wanakitaka chuo kuweka sera inayoelekeza ni namna gani kitawawezesha kupata kiwango hicho cha elimu badala ya kuacha jukumu hilo liwe la wao binafsi."Hivi karibuni katika ripoti yake iliyowasilishwa kwenye Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU), UDSM ilieleza kuwa kuna mafunzo kwa ajili ya wafanyakazi wake, lakini utoaji wa PhD haukuelezwa kama eneo muhimu," ilisema sehemu ya taarifa ya mkutano huo.

Wakati idadi ya wahadhiri wasaidizi wanaoajiriwa imepanda kwa kiwango kikubwa kutoka 22 wa mwaka 2001/02 hadi wahadhiri wasaidizi 78 wa 2005/06, lakini idadi ya wahadhiri hao wanaofuzu PhD imeshuka kutoka 78 wa miaka mitano iliyopita hadi kufikia 28 .Wakielezea mazingiraya ya chuo, walisema ni mabovu si tu kwao pekee, bali pia kwa wanafunzi kiasi cha kutishia mustakhabali wa elimu. Walinyooshea vidole hali ya ubaguzi uliopo kati yao na wahadhiri wakongwe na wafanyakazi wengine wa utawala wakongwe na hususan katika upatikanaji wa huduma za jamii.

Walitoa mfano juu ya ukosefu wa fedha za kujikimu kwa waajiriwa wapya. Kwa upande wa nyumba, walisema wanataaluma wachanga wengi hawapewi nyumba. Walisema ni wachache waliopewa nyumba ama ndani ya kampasi au nje ya chuo.

Walisema wakati wahadhiri waandamizi (senior lecturers) na wafanyakazi wengine wa utawala hupewa posho ya pango, wahadhiri hao wachanga licha ya kutopewa nyumba, vile vile hawapewi posho hiyo huku wachache wanaopewa nyumba, wakikatwa asilimia 10 ya mshahara.Wakizungumzia matatizo ya wanafunzi, waliomba mamlaka zinazohusika kufanya juhudi za makusudi za kuboresha mazingira ya kujifunzia. Walisema ni makosa kwa UDSM kujiondoa katika utoaji wa huduma za kijamii kwa wanafunzi .

"Haiwezekani mafunzo yakafanikiwa kwa wanafunzi wenye matatizo ya kisaikolojia yanayotokana na ukosefu wa mazingira mazuri ya kusomea na tatizo la makazi." Walishutumu kuwa maboresho yanayoendelea chuoni hapo yanalenga kuongeza idadi ya wanafunzi badala ya kuboresha hali zao.Walisema pamoja na vipingamizi vya kifedha ambavyo vimekuwa vikitajwa kuwa vinakwamisha juhudi za kuboresha hali ya wanafunzi na wafanyakazi, lakini bado kuna udhaifu katika matumizi ya fedha kidogo zilizopo.

Ilielezwa kuwa kuna hitilafu kubwa katika vipaumbele vya kushughulikia masuala mbalimbali chuoni hapo. Ulitolewa mfano kuwa haiingii kichwani kuwa chuo kinaweza kukosa fedha za kuwalipa wafanyakazi wake wanaoandaa mitihani mchana na usiku, lakini kikaweza kulipa sh7milioni kama posho ya kikao cha dakika 30.

"Cha kushangaza ni kwamba wanaolipwa hiyo posho, ni waajiriwa wa chuo hiki hiki ambao huacha kufanya kazi zao kwa ajili ya kuhudhuria mikutano," inasema taarifa ya wahadhiri hao.Wakizungumza na gazeti hili, waratibu wa mkutano huo, Bashiri na Mkumbo walisema wanataaluma hao wameazimia kuendeleza jukwaa hilo la mjadala kwa ajili ya kubadilishana mawazo juu ya ufanisi wao chuoni hapo


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.