Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Swissport yalalamikiwa na wafanyakazi
Swissport yalalamikiwa na wafanyakazi
By Habari Tanzania | Published  09/23/2006 | Habari za Kitaifa | Rating:
Christina Gregory na Amana Nyembo

KAMPUNI ya Swissport inalalamikiwa na Umoja wa Wafanyakazi wa Chama cha Mawasiliano na Uchukuzi Tanzania (COTWU –T) kwa kuwanyonya kutokana na mshahara wanaopata ambao wanadai haulingani na kazi wanayoifanya.

Mwenyekiti wa COTWU-T, George Faustine, aliyasema hayo juzi Dar es Saalaam kwenye kikao kilichowahusisha wanachama wa chama hicho.

Faustine alisema kampuni hiyo imekuwa ikifanya baadhi ya mambo bila kuwashirikisha wafanyakazi, likiwamo suala la mikataba kati ya wafanyakazi na waajiri.

Alisema wafanyakazi wa kampuni hiyo wamekuwa wakifanya kazi muda wa ziada lakini malipo yake hayawi sahihi kutokana na muda wanaofanyia kazi.

Alisema wafanyakazi wanapata matatizo katika usafiri kwani kuna baadhi ya wafanyakazi wanarudishwa nyumbani na gari na wengine hawarudishwi wakati wote wametoka muda mmoja, iwe mchana au usiku.

“Utakuta mfanyakazi wa kike anakaa mbali na ametoka kazini usiku lakini akiomba usafiri hapewi, sasa mtu kama huyu anaweza kupatwa na tatizo njiani na ikawa taabu kwa familia yake,” alisema.

Hata hivyo mwenyekiti huyo aliwataka wafanyakazi wake wafuate maadili ya kazi, wasije kazini wakiwa wamelewa, kwani watakuwa wamevunja maadili ya kazi.

Akijibu malalamiko hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Swissport, Gaudence Temu, alisema wafanyakazi wamekuwa wakilipwa kutokana na sifa na utendaji kwa kuangalia vigezo, kwani mbeba mizigo hawezi kulipwa sawa na anayeangalia uzito wa ndege.

“Kwa upande wa usafiri, wote wanachukuliwa na basi na kurudishwa, hakuna mtu anayebaguliwa, tuwabague ili iweje?” alihoji.

Alisema kwa upande wa matibabu, kila mtu anatibiwa kutokana na mfuko wake na hakuna ubaguzi katika suala hilo, kwani wafanyakazi wa mikataba wapo katika mfuko wa NSSF na wale wa kudumu wapo chini ya PPF, na kila mfuko una utaratibu wa matibabu kwa watu wake. Temu alisema kampuni inafuata misingi ya utawala bora, hivyo hakuna ubaguzi unaofanywa kati ya wafanyakazi hao.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.