Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Noti bandia Magomeni
Noti bandia Magomeni
By Habari Tanzania | Published  09/23/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated
na Mwandishi Wetu

GENGE la wahalifu limeibuka jijini Dar es Salaam, likijihusisha na utengenezaji wa noti bandia, Tanzania Daima imebaini.

Wahusika wa uhalifu huo wapo Mtaa wa Mkadini, Magomeni, jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya watu wameiambia Tanzania Daima kuwa wahalifu hao wana mtambo wa kutengeneza fedha za Tanzania na Kenya.

Suala hilo limeshafikishwa katika vyombo vya dola, lakini hakuna dalili za kulishughulikia kwa lengo la kulitokomeza.

Baadhi ya viongozi eneo la Magomeni walioomba majina yao yahifadhiwe, wamethibitisha kuwapo kwa uhalifu huo, na kushangaa kasi ya polisi ya kulimaliza tatizo hilo.

Walisema pamoja na utengenezaji wa noti bandia, pia kumeshamiri biashara ya mihadarati.

Baadhi ya watuhumiwa, wameamriwa kulihama eneo hilo.

Mmoja wa waliokuwa wadaiwa wa biashara hiyo, alisema noti ya sh 10,000 hununuliwa na walanguzi kwa sh 3,000.

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilishakataa kata kata kuwa noti za sasa haziwezi kughushiwa kirahisi.

Hata hivyo, Jeshi la Polisi, kupitia kwa aliyekuwa msemaji wake, Aden Mwamunyange, lilisisitiza kuwa noti bandia zipo mitaani, na kwamba ushahidi upo.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.