Kitaifa
   Siasa
   Jamii
   Uchumi
   Makala

 

Search


Advanced Search

 »  Home  »  Habari za Kitaifa  »  Tanapa yakana kutoza kodi watalii
Tanapa yakana kutoza kodi watalii
By Habari Tanzania | Published  09/21/2006 | Habari za Kitaifa | Unrated

Na Mussa Juma, Arusha
MAMLAKA ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), imesema haihusiki na kodi wanazotozwa watalii na wabeba mizigo katika eneo la msitu wa West Kilimanjaro, wakiwa njiani kupanda Mlima Kilimanjaro kupitia njia ya Lemosho.

Afisa Uhusiano wa TANAPA, Catherine Mbena alisema, mamlaka hiyo haina uhusiano na kodi hizo kwa kuwa ina kodi zake ambazo zinalipwa na watalii na wabeba mizigo hao.

"Sisi hatufahamu hilo ila naomba uwasiliane na watu wa misitu au maafisa wa Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro, KINAPA kama wanalijua hilo, " alisema Mbena.

Afisa mmoja wa KINAPA , hata hivyo alisema hata wao hawalitambui hilo.

Kwa zaidi ya miezi mitatu sasa, maafisa wa msitu wa West Kilimanjaro, wamekuwa wakilalamikiwa na kampuni za utalii kwa kudai malipo ya Sh5,000 kwa kila mtalii anayepita katika msitu huo kwenda kupanda Mlima Kilimanjaro na Sh3,000 kwa kila mbeba mizigo.

Kwa kawaida mtalii mmoja husaidiwa na wabeba mizigo si chini ya watano, zoezi zima la kupanda Mlima Kilimanjaro huchukuwa wastani wa siku saba .

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Chama cha Makampuni ya Utalii (TATO), Mustapha Ukuunay alisema anachofaumu malipo hayo yamefutwa.

Hata hivyo, Meneja Misitu hifadhi Mkoa wa Kilimanjaro, Julius Mkumbo, alisema kodi hizo ingawa zinalalamikiwa, zinatozwa kisheria na wao kama watekelezaji hawawezi kwenda kinyume na maagizo tofauti zaidi ya kudai fedha hizo.

"Sheria hii ipo wazi kwa mgeni anayepita katika eneo la hifadhi ya misitu anapaswa kulipa dola 5 na mtanzania ambaye anaingia kutembea au kufanya utafiti anapaswa kulipa Sh3,000,"alisema Mkumbo.

Alisema sheria hiyo ya misitu ya mwaka 2002 katika kanuni za sheria, kipengele C sehemu ya pili inaeleza wazi kukusanywa kwa fedha hizo za serikali.


How would you rate the quality of this article?
1 2 3 4 5
Poor Excellent
Add comment
Comments


Article Options
Your Favorite Articles
View All Favorites
Articles to Read
You Recently Viewed...
Popular Articles
  1. Unaifahamu Jambo Forums?
  2. Barua ya Wazi kwa Rais Jakaya Kikwete
  3. Ghorofa Jijini lanusurika kuungua moto
  4. Is Tanzania a safe place to invest?
  5. Britsh M.P. calls for the suspension of aid to Tanzania.
No popular articles found.
Popular Authors
  1. Habari Tanzania
  2. Mzee Mwanakijiji
  3. Marshy Abdu
  4. Linda Garner
  5. Nthelezi Nesaa
  6. Prosper Kwigize
  7. Ramadhan Semtawa
  8. Salehe Mmoro
  9. Manyerere Jackton
  10. Ndesanjo Macha
No popular authors found.